ⓘ Free online encyclopedia. Did you know? page 57
                                               

Konstantin Chernenko

Konstantin Ustinovich Chernenko alikuwa mwanasiasa wa Urusi na Katibu Mkuu wa tano wa Chama cha Kikomunisti cha Umoja wa Kisovyeti. Aliongoza Umoja huo kutoka 13 Februari 1984 hadi kifo chake tarehe 10 Machi 1985.

                                               

Lars Korvald

Lars Korvald alikuwa mwanasiasa kutoka nchi ya Norwei. Alikuwa Waziri Mkuu wa Norwei kuanzia 17 Oktoba 1972 hadi 12 Oktoba 1973.

                                               

Nikita Krushchov

Nikita Sergeyevich Krushchov alikuwa kiongozi wa Umoja wa Kisovyeti baada ya kifo cha Joseph Stalin. Alitawala kati ya 1953 hadi 1964. Krushchov alizaliwa mjini Kalinovka, Urusi. Baadaye alihamia Ukraine. Alikuwa mfanyakazi wa migofi akajiunga na ...

                                               

Leonid Brezhnyev

Leonid Ilyich Brezhnyev alikuwa mwanasiasa wa Urusi ambaye aliongoza Umoja wa Kisovyeti kama Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti kinachotawala na kama Mwenyekiti wa Uenezi wa Sovie Kuu. Muhula wake wa miaka 18 kama katibu mkuu ulikuwa wa pili ba ...

                                               

Ruud Lubbers

Rudolphus Franciscus Marie "Ruud" Lubbers alikuwa mwanasiasa nchini Uholanzi. Alikuwa Waziri Mkuu wa Uholanzi kuanzia 4 Novemba 1982 hadi 22 Agosti 1994. Kuanzia 1 Januari 2001 hadi 20 Februari 2005 alikuwa afisa kwa wakimbizi chini ya Umoja wa M ...

                                               

Rosa Luxemburg

Rosa Luxemburg alikuwa mwanasiasa na mwanafalsafa kutoka Poland aliyeishi muda mrefu Ujerumani. Alizaliwa katika familia ya Wayahudi katika sehemu ya Poland iliyokuwa sehemu ya milki ya Urusi. Tangu utoto alijiunga na vikundi vya kisoshalisti wal ...

                                               

John Lyng

John Daniel Lyng alikuwa mwanasiasa kutoka nchi ya Norwei. Alikuwa Waziri Mkuu wa Norwei kuanzia tarehe 28 Agosti hadi 25 Septemba 1963. Tena alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje miaka ya 1965-1970.

                                               

Niccolo Machiavelli

Niccolo Machiavelli alikuwa mwanasiasa, mwandishi na mwanafalsafa nchini Italia. Machiavelli anajulikana duniani kwa maandishi yake ambamo alieleza siasa kama mbinu ya kutafuta na kutetea utawala bila kujali maadili au tofauti kati ya mema na mabaya.

                                               

Ephraim Nehemia Madeje

Ephraim Nehemia Madeje ni mbunge wa Tanzania katika jimbo la uchaguzi la Dodoma mjini alipochaguliwa mwaka 2005 kama mgombea wa CCM kwa asilimia 91 za kura zote. Madeje ni mzaliwa wa kijiji cha Buigiri. Alisoma BA ya uchumi kwenye Chuo Kikuu cha ...

                                               

Mahmud II

Mahmud II alikuwa Sultani wa 30 wa Milki ya Osmani aliyetawala miaka 31 kuanzia 1808 hadi kifo chake. Mahmud alikuwa mwana wa Sultani Abdül Hamid I. Wakati wake kama sultani inakumbukwa kwa kutoka kwa Ugiriki na Serbia katika utawala wa Kiosmani, ...

                                               

Maktoum bin Rashid Al Maktoum

Maktoum bin Rashid Al Maktoum Maktūm bin Rāshid al-Maktūm pia anajulikana kama Sheikh Maktoum alikuwa Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu na Emir au mtawala wa Dubai. Mzaliwa wa Al Shindagha, Dubai kwa familia ya Al Maktoum ...

                                               

Rashid Bin Saeed Al Maktoum

Kigezo:Infobox prime minister Sheikh Rashid Bin Saeed Al Maktoum alikuwa Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu na Emir wa Dubai. Yeye alitawala kwa miaka 32, mpaka kifo chake. Sheikh Rashid Bin Saeed Al Maktoum anaweza kuitwa ...

                                               

Malcolm X

Malcolm X jina lake la awali lilikuwa Malcolm Stuart Little ; 19 Mei, 1925 - 21 Februari 1965 alikuwa mwanaharakati wa haki za kiraia za Waafrika-Waamerika na haki za kiraia kwa jumla. Baba ya Malcolm X alikuwa mchungaji wa Kibatisti ambaye ngozi ...

                                               

John Samwel Malecela

John Samwel Malecela ni mbunge wa jimbo la Mtera katika bunge la kitaifa huko nchini Tanzania. Anatokea katika chama cha CCM. Pia alishawahi kuwa Naibu Mwenyekiti wa CCM, Waziri Mkuu, Kamishina Mkuu wa Tanzania huko Uingereza, Waziri wa Utamaduni ...

                                               

Malkia Cixi

Malkia Cixi wa China alikuwa mwanamke Mchina aliyeshika utawala wa China kwa miaka mingi wakati wa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20. Cheo chake rasmi kilikuwa mjane wa kaisari akatawala kwa kushika mamlaka kwa niaba ya Kaisari wa nasaba ya ...

                                               

Mange Kimambi

Mange Jumanne Ramadhan Kimambi ni mmoja wa wanawake wanaharakati wenye ushawishi mkubwa katika nchi ya Tanzania. Mange Kimambi kabila lake ni Mpare. Ameolewa na Mzungu raia wa Marekani na wamebahatika kupata watoto wawili wa kiume. Hadi sasa amek ...

                                               

Mao Zedong

Mao Zedong alikuwa kiongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China tangu 1935 hadi kifo chake na pia kiongozi mkuu wa China tangu 1949. Aliongoza wakomunisti katika vita dhidi ya jeshi la Japan wakati wa vita kuu ya pili ya dunia na katika vita vya w ...

                                               

Mathieu Kérékou

Mathieu Kérékou alikuwa mwanasiasa wa Benin ambaye alikuwa Rais wa nchi kutoka mwaka 1972 hadi 1991, tena kutoka 1996 hadi 2006. Baada ya kushika madaraka kwa mapinduzi ya kijeshi, alitawala nchi hiyo kwa miaka 19, kwa zaidi ya hiyo wakati chini ...

                                               

Kenneth Matiba

Kenneth Matiba alikuwa mwanasiasa wa Kenya aliyeibuka wa pili katika uchaguzi wa urais mwaka 1992. Mwaka 2007 alitangaza kwamba alinuia kuwania urais kama mgombea huru. Aliibuka wa saba akipata kura 8.046.

                                               

Maximilien de Robespierre

Maximilien François Marie Isidore de Robespierre alikuwa mwanasheria na mwanasiasa wa Ufaransa mwenye ushawishi mkubwa katika Mapinduzi ya Kifaransa na Utawala wa Hofu. Kama mwanachama wa Waziri Mkuu, Bunge la Kimbunge na Klabu Ya Jacobin, Robesp ...

                                               

John McCain

John Sidney McCain III alikuwa mwanasiasa wa Marekani akiwa mwanachama wa Chama cha Jamhuri. Tangu mwaka 1987 hadi kifo chake alikuwa mbunge wa Senati ya Marekani akiwakilisha jimbo la Arizona. Mwaka wa 2008 aligombea urais lakini akashindwa na B ...

                                               

George McGovern

George Stanley McGovern alikuwa mwanasiasa wa Marekani akiwa mwanachama wa Chama cha Kidemokrasia. Kuanzia 1963 hadi 1981 alikuwa mbunge wa Senati ya Marekani akiwakilisha jimbo la South Dakota. Mwaka wa 1972 aligombea urais lakini akashindwa na ...

                                               

Melchior Ndadaye

Melchior Ndadaye alikuwa msomi wa sayansi na mwanasiasa. Yeye alikuwa wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia na wa kwanza wa kabila la Wahutu kuwa rais wa Burundi baada ya kushinda uchaguzi kuu wa kihistoria mwaka 1993. Ingawa alijaribu kukomesha uka ...

                                               

Mariam Salum Mfaki

Mariam Salum Mfaki alikuwa mwanasiasa wa Tanzania. Aliwahi kua Mbunge wa viti maalumu wa Bunge la Tanzania jijini Dodoma tangu mwaka 2000 mpaka alipofariki mwaka 2015. Mfaki alianza kujihusisha na siasa akiwa kama katibu wa umoja wa wanawake wa C ...

                                               

Slobodan Milosevic

Slobodan Milosevic alikuwa Rais wa Serbia kuanzia mwaka 1989 hadi 2000. Pia alikuwa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Yugoslavia kutoka 1997 hadi 2000. Aliongoza Chama cha Kijamaa cha Serbia kutoka msingi wake mnamo 1990 na aliibuka na kuwa Rais w ...

                                               

Benjamin Mkapa

Benjamini William Mkapa alikuwa Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, CCM.

                                               

Morgan Tsvangirai

Morgan Richard Tsvangirai alikuwa mwanasiasa wa Zimbabwe ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa Zimbabwe kutoka mwaka 2009 hadi 2013. Alikuwa Rais wa Harakati ya Kidemokrasia ya Kidemokrasia, na baadaye Harakati za Harakati za Kidemokrasia - Tsvangirai, n ...

                                               

Hosni Mubarak

Muhammad Hosni Said Mubarak b alikuwa rais wa Misri kuanzia 14 Oktoba 1981 hadi 11 Februari 2011. Mubarak alikuwa mmoja wa watawala wenye mamlaka na nguvu zaidi kwenye eneo la Mashariki ya kati. Alifuata siasa ya rais mtangulizi Sadat aliyepatana ...

                                               

Muhammad Ali Pasha

Kwa watu wengine wenye jina hili tazama Muhammad Ali Muhammad Ali Pasha kwa Kiarabu محمد علي باشا, Februari 1769 - 2 Agosti 1849 alikuwa mwanajeshi wa Milki ya Osmani aliyeendelea na kuwa mtawala wa Misri na Sudan. Hata kama alipaswa kukubali ras ...

                                               

Kalonzo Musyoka

Alijiunga na siasa katika chama cha KANU akachaguliwa kuwa mbunge mara ya kwanza 1985 katika uchaguzi mdogo wa Kitui-North baadaye Mwingi-North. 1986 alipewa kazi ya waziri msaidizi katika wizara ya kazi za umma.

                                               

Aboud Jumbe Mwinyi

Aboud Jumbe Mwinyi alikuwa rais wa pili wa Zanzibar toka tarehe 11 Aprili 1972 hadi 29 Januari 1984 alipojiuzulu.

                                               

Nana Akufo-Addo

Nana Addo Dankwa Akufo-Addo ni mwanasheria na mwanasiasa wa chama cha NPP nchini Ghana. Tangu tarehe 9 Desemba 2016 ni rais mteule wa nchi baada ya kushinda uchaguzi dhidi ya rais mtendaji John Dramani Mahama. Akufo-Addo alikuwa anagombea urais w ...

                                               

Nicolas Grunitzky

Nicolas Grunitzky alikuwa rais wa pili wa Togo na mkuu wa nchi wa tatu. Alikuwa Rais kuanzia 1963 hadi 1967. Grunitzky alikuwa Waziri Mkuu wa Togo 1956-1958 chini ya Kifaransa Colonial loi kada mfumo, ambayo kuundwa mdogo "kitaifa" serikali katik ...

                                               

Simeon Nyachae

Alizaliwa katika kata ndogo ya Nyaribari, Wilayani Kisii Mkoani Nyanza. Amehudumu katika nyadhifa mbali katika serikali za Kenyatta, Moi na Kibaki. Kwa miaka mingi Nyachae alionekana kama kiongozi wa Kisii hadi alipongatuliwa kutoka bungeni katik ...

                                               

Julius Nyerere

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa rais wa kwanza wa Tanzania, na mara nyingi anatajwa kama "Baba wa Taifa" kwa jinsi alivyoathiri nchi hiyo. Ndiye mwasisi wa itikadi ya ujamaa na kujitegemea iliyotangazwa hasa katika Azimio la Arusha. Kabl ...

                                               

Jaramogi Oginga Odinga

Jaramogi Ajuma Oginga Odinga alikuwa mwalimu, mfanyabiashara, mwanasiasa na kiongozi wa Waluo nchini Kenya. Alikuwa makamu wa rais wa kwanza wa Kenya.

                                               

Oliver Cromwell

Oliver Cromwell alikuwa mwanajeshi na mwanasiasa wa Uingereza. Anajulikana kwa kufanya jamhuri ya Uingereza kuwa na umoja na soko la pamoja. Cromwell alikuwa mwanamapinduzi ambaye alikuwa akipinga utawala wa mfalme Charles I wa Uingereza ambaye a ...

                                               

Peterson Munuhe Kareithi

Alizaliwa kwenye kijiji cha Mbari-ya-Hwai, katika Kaunti ya Nyeri. Alisomea shule ya Tumutumu na hatimaye kwenda shule ya Kagumo TTC, ambapo alihitimu kupata shahada ya ualimu wa shule za msingi. Alianza kufundisha mnamo 1954 huku akijieleimisha ...

                                               

Pio Gama Pinto

Akiwa na umri wa miaka nane, yeye alipelekwa India kusoma na alitumia miaka tisa iliyofuata huko. Alisoma sanaa kwa miaka miwili kabla ya kujiunga na Jeshi la Anga la India mwaka wa 1944 kwa muda mfupi. Akiwa na miaka kumi na saba, akaanza kuupin ...

                                               

Qabus bin Said al Said

Qabus bin Said al Said alikuwa Sultani wa Oman tangu mwaka 1970 hadi 2020. Alikuwa kizazi cha kumi na nne cha mwanzilishi wa Jumba la Al Said. Alikuwa kiongozi aliyehudumu miaka mingi katika Mashariki ya Kati na Ulimwengu wa Kiarabu, akihudumu kw ...

                                               

Radama I

Mfalme Radama I alirithi kiti cha ufalme cha Andrianampoinimerina katika kisiwa cha Madagaska mwaka 1810 akiwa na umri wa miaka 18. Jukumu lake la kwanza kabisa baada ya kushika ufalme wa Merina lilikuwa kuyapiga makundi ya ndani ya ufalme huo ya ...

                                               

Radama II

Mfalme Radama II wa Wamerina kisiwani Madagaska alitawala miaka miwili tu, kati ya kifo cha mama yake, malkia Ravalona I na kifo chake mwenyewe. Shughuli zake zilielekezwa katika kuzibadilisha sera zote zilizokuwa zinapinga mambo yaliyoletwa na W ...

                                               

Ram Prasad Bismil

Ram Prasad Bismil alikuwa mwanamapinduzi wa India aliyeshiriki katika njama maarufu za Mainpuri mwaka 1918, na Kakori mwaka 1925. Alikuwa mpiganiauhuru dhidi ya wakoloni wa serikali ya Uingereza, pia alikuwa mshairi mzalendo aliyeandika katika lu ...

                                               

Ranavalona I

Malkia Ranavalona I wa Wamerina alikuwa binamu na mke wa kwanza wa mfalme Radama I, akatawala baada ya kifo cha mume wake hadi kifo chake mwenyewe. Kwa kuwa alisaidiwa kupata umalkia na makabila na wakuu wa majeshi ambao Radama aliwaondoa madarak ...

                                               

Robert Kennedy

Robert Francis Kennedy alikuwa mwanasiasa wa Marekani na mwanasheria ambaye alihudumu kama seneta wa Marekani kutoka New York tangu Januari 1965 mpaka kufa kwake. Alikuwa Mwanasheria wa Marekani wa 64 Mkuu kutoka Januari 1961 hadi Septemba 1964, ...

                                               

Robert Mugabe

Robert Gabriel Mugabe alikuwa kiongozi mkuu wa Zimbabwe tangu 1980 hadi 2017. Alikuwa mwenyekiti wa chama tawala cha ZANU. Mwaka 1980 alikuwa waziri mkuu na mwaka 1987 Rais wa Zimbabwe. Kabla ya wakati ule aliongoza upinzani wa ZANU dhidi ya seri ...

                                               

Walter Rodney

Walter Rodney 23 Machi 1942 - 13 Juni 1980 alikuwa mwanahistoria maarufu wa Guyana na mwanatakwimu wa kisiasa. Baada ya kuzaliwa katika familia ya wafanyakazi, Rodney alikuwa mwanafunzi mwerevu, na aliweza kuhudhuria Chuo cha Queens katika Guyana ...

                                               

Romano Prodi

Prodi aliwahi kuwa profesa wa uchumi kwenye Chuo Kikuu cha Bologna kati ya 1971 na 1999. Mwaka 1978 aliitwa na Waziri Mkuu Giulio Andreotti kujiunga na serikali yake kama waziri wa viwanda. Baada ya kuanguka kwa serikali hiyo mwaka 1979 Prodi ali ...

                                               

Saadani Abdu Kandoro

Saadani Abdu Kandoro alikuwa mwanasiasa na mshairi nchini Tanzania. Anahesabiwa kati ya wanasiasa waliopigania uhuru wa Tanganyika wakishirikiana na Julius Nyerere.

                                               

Salim Ahmed Salim

Salim Ahmed Salim ni mwanasiasa kutoka nchi ya Tanzania. Kuanzia tarehe 24 Aprili 1984 hadi tarehe 5 Novemba 1985 alikuwa Waziri Mkuu wa tano wa Tanzania. Alifuatwa na Joseph Sinde Warioba.