Back

ⓘ Pentekoste. Jina hili lilianza kutumika kwa sababu kwa lugha ya Kigiriki lina maana ya namba 50. Hivyo πεντηκοστή ni siku ya hamsini. ..
Pentekoste
                                     

ⓘ Pentekoste

Jina hili lilianza kutumika kwa sababu kwa lugha ya Kigiriki lina maana ya namba 50. Hivyo "πεντηκοστή) ni "siku ya hamsini".

                                     

1. Shavuot ya Kiyahudi

Sikukuu ya Kiyahudi ya Pentekoste inaadhimishwa siku ya hamsini baada ya Pasaka ya Kiyahudi. Sikukuu hii husherehekewa na Wayahudi pia kwa jina asili la Kiebrania חג השבועות, Hag ha Shavuot, yaani Sikukuu ya Majuma, kwa kifupi "shavuot" "majuma" jinsi ilivyoamriwa katika kitabu cha Mambo ya Walawi 23:16.

Ilikuwa sikukuu ya mavuno kama vile Pasaka ilivyohusiana na malimbuko.

                                     

2. Pentekoste ya Kikristo

Kwa wafuasi wa Yesu Kristo ni ukumbusho wa umwagaji wa Roho Mtakatifu juu ya mitume na wanafunzi wengine wa Yesu na kuanzishwa kwa Kanisa siku ya 50 baada ya Pasaka ya Kikristo au ufufuko wa Yesu.

Inawezekana kusema ya kuwa baada ya kifo na ufufuko wa Yesu wanafunzi wake - ambao walikuwa wote Wayahudi - walikutana kwenye sikukuu ya Kiyahudi ya Shavuot wakati ambapo Wayahudi kutoka nchi mbalimbali walipotembelea Yerusalemu kwa hija kwenye nafasi ya sikukuu ile.

Tangu kuachana kwa kalenda ya Kikristo na kalenda ya Kiyahudi sikukuu zake kwa kawaida haziangukii siku ileile tena.

                                     

3. Pentekoste ya Mitume

Maelezo juu ya Pentekoste ya kwanza ya Kanisa hupatikana katika sura ya pili ya kitabu cha Matendo ya Mitume cha Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo.

Humo Mwinjili Luka anasimulia jinsi wanafunzi wa Yesu walivyokutana katika mji wa Yerusalemu siku ile ya "Pentekoste" na kupokea paji la Roho Mtakatifu. Baadaye walitoka nje ya nyumba ya ghorofa walimokaa, wakianza mara kuhubiri juu ya Yesu Kristo mbele ya watu wengi, wakiwa wakazi wa mji huo pamoja na wageni kutoka nchi nyingi.

Kufuatana na taarifa yake siku hiyo watu takriban 3.000 walibatizwa kwa jina la Yesu na kuongezeka katika kile kikundi. Ndiyo maana Pentekoste inahesabiwa kuwa kuzaliwa kwa Kanisa.

                                     

4. Tarehe ya Pentekoste

Husherehekewa jumapili ya 7 baada ya Pasaka.

Katika madhehebu ya Ukristo yanayofuata kalenda ya Gregori Pentekoste itasherehekewa kwenye tarehe zifuatazo:

 • 2016: 15 Mei
 • 2017: 4 Juni
 • 2015: 24 Mei
 • 2020: 31 Mei
 • 2019: 9 Juni
 • 2018: 20 Mei

Makanisa ya Kiorthodoksi yanayofuata kalenda ya Juliasi huwa na tarehe tofauti.

                                     

5. Madhehebu ya Kipentekoste

Kuanzia mwaka 1907, katika Ukristo limejitokeza tapo la kiroho linalosisitiza umuhimu wa karama kama zilivyojitokeza siku ya Pentekoste na mwanzoni mwa Kanisa. Ndiyo sababu waumini wake wanaitwa Wapentekoste.

                                     
 • siku inayotangulia Jumatano ya Majivu, halafu kuanzia Jumatatu baada ya Pentekoste hadi mchana wa Jumamosi ya tarehe yanapoanza kuadhimishwa Majilio. Katikati
 • Sherehe yake huadhimishwa Ijumaa inayofuata Jumapili ya pili baada ya Pentekoste kati ya tarehe 29 Mei na 2 Julai. Jinsi ilivyo kwa sasa imetokana hasa
 • linalolenga kuleta upyaisho katika Kanisa kwa kutia maanani tukio la sikukuu ya Pentekoste ya mwaka uleule wa kifo na ufufuko wa Yesu. Tapo hilo linaungana na Waprotestanti
 • maadhimisho mbalimbali, kama vile yale muhimu zaidi ya Kipindi cha Pasaka hadi Pentekoste na hata nje yake, kwa mfano wakati wa ubatizo na mazishi ya Kikristo
 • ufufuko Aprili 30 au 33 Roho Mtakatifu alidhihirika kwa kishindo kwenye Pentekoste ya mwaka ule Mdo 2: 1 - 11 haohao na wengineo walipokuwa wakimngojea wakisali
 • Ukristo ndio wenye asilimia kubwa, kwani kuna Ukatoliki, Anglikana, Sabato, Pentekoste PAG, TAG, EAGT, PEFA, FPTC Moravian n.k. Kata ina kanisa kubwa la Katoliki
 • kwa njia ya Roho Mtakatifu aliyetumwa naye juu ya Mitume wake siku ya Pentekoste mwaka 30 au 33 BK. Ni imani inayoungamwa katika ubatizo, sakramenti
 • wa Yohane nawe utaitwa Kefa tafsiri yake Petro Yoh 1: 42 Siku ya Pentekoste waliolipokea neno lake wakabatizwa na siku ile wakaongezeka watu wapata
 • kifo chao wote. Habari kuu za kipindi cha kwanza, kama ile ya siku ya Pentekoste Roho Mtakatifu kuwashukia wafuasi wa Yesu, zinapatikana hasa katika Matendo
 • kháris neema Neno hilo limekuwa likitumika sana katika Kanisa kuanzia Pentekoste na katika barua za Mtume Paulo, kwa msisitizo kuwa karama zote zinamtegemea
 • katika liturujia ya madhehebu mbalimbali ya Ukristo wa mashariki siku ya Pentekoste na ya Ukristo wa magharibi Jumapili inayofuata 2012 The Oxford Handbook
 • Sakramenti hizo ni kama pande mbili za pesa moja. Zinahusiana kama Pasaka na Pentekoste ambayo ni utimilifu wake, kwa kuwa siku alipofufuka Yesu aliwapulizia
 • Pasaka: ndiyo sikukuu yenyewe ambayo inadumu siku hamsini mfululizo hadi Pentekoste na inaitwa Dominika kubwa. Kwa kweli Pasaka si sherehe mojawapo tu wala

Users also searched:

...

Ndoto Yangu ya Ufalme wa Mwenyezi Mungu ni Mchungaji Wangu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Ibada ya jumapili Dominika ya sherehe ya Pentekoste. Ndoto Yangu ya Ufalme wa Kibinguni Kanisa la Mwenyezi Mungu. KANISA LA PENTEKOSTE ARUSHA KLPA lilianzinshwa hapa nchini na Waminisionari kutoka Sweden mnamo mwaka 1958, kanisa liliendelea mpaka tarehe. Viongozi wa Madhehubu Mengine Bukoba Catholic Diocese. Makanisa mawili WinnerS Chapel na Pentekoste Assembly of God, Msikiti, Shule za Msingi mbili, Zamzam na Bilele, barabara za Kashozi na Kashai pamoja.


...