Back

ⓘ Historia ya Visiwa vya Karibi inaeleza ramani ya kisasa ya eneo hili na mchanganyiko wa lugha na tamaduni unaopatikana kwenye visiwa hivyo vilivyopo kati ya Ame ..
Historia ya Visiwa vya Karibi
                                     

ⓘ Historia ya Visiwa vya Karibi

Historia ya Visiwa vya Karibi inaeleza ramani ya kisasa ya eneo hili na mchanganyiko wa lugha na tamaduni unaopatikana kwenye visiwa hivyo vilivyopo kati ya Amerika ya Kusini na Amerika ya Kaskazini.

                                     

1. Kabla ya mawasiliano na Ulaya

Miaka 10.000 - 12.000 iliyopita vikundi vya wawindaji na wavuvi walikuwa wamefika Amerika ya Kusini na kusambaa katika bara. Wengi wao walikuwa hawajaanza bado kujenga makazi ya kudumu bali walihamahama.

Trinidad ilikuwa kisiwa cha kwanza cha Karibi kilichofikiwa na wanadamu takriban mnamo 9000/8000 KK ilhali wakati ule iliunganishwa bado na bara kwa nchi kavu. Makazi ya kale ya miaka ya 6000 KK hadi 5100 KK yalitambuliwa pale St. Johns ambako mafungu makubwa ya kombe za kome yamegunduliwa yaliyokuwa chakula chao.

Visiwa vingine nje ya Trinidad vilianza kufikiwa na watu kuanzia miaka ya 3000 KK na akiolojia imegundua mabaki ya kipindi hicho huko Barbados, Kuba, Curaçao na St Martin, ikifuatiwa na Hispaniola na Puerto Rico.

Kati ya miaka 800 na 200 KK kilitokea kikundi kipya cha wahamiaji kwenye visiwa ambao wanatambuliwa kutokana na vyungu vyao vya pekee.

Kipindi cha miaka 650 hadi 800 BK kiliona mabadiliko makubwa ya kitamaduni, kijamii na kisiasa ambayo yalitokea bara na katika visiwa vingi vya Karibi. Kipindi hicho kilikuwa na mabadiliko ya hali ya hewa. Vipindi vya ukame viliongezeka, pamoja na kutokea kwa vimbunga. Kwa jumla idadi ya watu wa Karibi iliongezeka na jamii zilibadilika kutoka makazi katika kijiji kimoja hadi kuunda marundiko ya vijiji. Kilimo kwenye visiwa kiliongezeka.

Wakati wa kuwasili kwa Wazungu, makundi makubwa matatu ya Waindio waliishi visiwani:

 • Wakaribi wa visiwa na Wagalibi katika Visiwa vya Windward ;
 • Wataino waliitwa pia Waarawak katika Antili Kubwa, Bahamas na Visiwa vya Leeward;
 • Wasibonei magharibi mwa Kuba.
 • Wataino wamegawanywa katika Wataino wa Kawaida, ambao walichukua Hispaniola na Puerto Rico, Wataíno wa Magharibi, ambao walichukua Cuba, Jamaica, na visiwa vya Bahamas, na Wataino wa Mashariki, ambao walichukua Visiwa vya Leeward. Trinidad ilikaliwa na vikundi vyote vinavyozungumza Wakaarib na Arawak.
                                     

2. Mwanzo wa ukoloni

Mara tu baada ya safari za Christopher Columbus kwenda Amerika alipotua kwenye eneo la Karibi mara ya kwanza mwaka 1492, Hispania na Ureno zilituma jahazi zao kwa upelelezi zaidi na kuanza kudai utawala juu ya maeneo. Baada ya kugunduliwa kwa dhahabu katika visiwa kadhaa, pia mataifa mengine ya Ulaya, hasa Uingereza, Uholanzi na Ufaransa zilitarajia kuanzisha makoloni yenye faida. Mashindano ya nchi hizo yalisababisha vita kati ya milki za Ulaya kwa karne kadhaa zilizopigwa pia kwenye makoloni yao.

Mwanzo wa karne ya 19 uliona harakati ya makoloni mengi ya Hispania katika Amerika ya Kusini kupigania uhuru na himaya ya kikoloni ya Hispania iliporomoka. Lakini Kuba na Puerto Rico zilibaki chini ya taji la Hispania hadi Vita ya Marekani dhidi Hispania ya mwaka 1898.

                                     

2.1. Mwanzo wa ukoloni Uvamizi wa Hispania

Wakati wa safari ya kwanza ya Christopher Kolumbus mawasiliano yalifanywa na wenyeji katika Bahamas na Wataíno huko Kuba waliokuwa na mapambo ya dhahabu. Dhahabu hiyo iliwahamasisha Wahispania kutafuta utajiri wakiwalazimisha wenyeji kuchimba metali hiyo adimu. Waindio walianza kufa, pamoja na ukali wa Wahispania hasa kutokana na maambukizo ya magonjwa kutoka Ulaya ambayo hayakujulikana awali upande huo wa bahari.

Hapo Wahispania walianza kuleta watumwa Waafrika, kwa imani kwamba hawataathiriwa na magonjwa hayo. Pia mapadre wa Kanisa Katoliku walishawishi wafalme wa Hispania kutangaza sheria zilizoweka vikwazo kwa utumwa wa Waindio. Ndio chanzo cha wakazi wengi wa Visiwa vya Karibi kuwa na asili wa Afrika. Watumwa walichukuliwa kwa kazi katika migodi na pia kwenye mashamba, hasa mashamba ya miwa ambayo ilikuwa zao lisilostawi katika sehemu kubwa ya Ulaya.

Hispania ilidai utawala juu ya visiwa vyote lakini kulikuwa na makazi kwenye visiwa vikubwa vya Hispaniola, Puerto Rico, Jamaika, Kuba na Trinidad pekee, ilhali waliacha visiwa vingi vidogo.                                     

2.2. Mwanzo wa ukoloni Utumwa

Kustawi kwa kilimo kwenye visiwa vya Karibi kulihitaji wafanyakazi wengi. Wazungu walitumia nafasi ya upatikanaji wa watumwa barani Afrika. Biashara ya watumwa ya Atlantiki ilileta watumwa wa Kiafrika katika makoloni ya Uingereza, Uholanzi, Ufaransa, Ureno na Hispania katika Amerika, pamoja na visiwa vya Karibi.

Jedwali lifuatalo linaorodhesha idadi ya watumwa walioletwa katika baadhi ya makoloni ya Karibi:

Wapinzani wa utumwa abolutionists katika Amerika na huko Ulaya, hasa Uingereza walianza kupinga unyama wa utaratibu huo tangu mwisho wa karne ya 18. Uingereza ilitangaza sheria ya kukataza biashara ya watumwa kwenye mwaka 1807 ikafaulu kuingiza ukomeshaji wa biashara ya watumwa kuvukia bahari katika maazimio ya Mkutano wa Vienna wa 1815. Marekani ilikuwa pia na sheria ya kukataza kuchukuliwa kwa watumwa kutoka nje tangu mwaka 1807. Usafirishaji wa watumwa kutoka milki za Afrika ulipungua, ingawa bado kulikuwa na magendo ya watumwa kutoka Afrika.

Hata hivyo, katika miongo ya kwanza utumwa uliendelea kwa hao waliokuwepo upande wa Amerika na waliozaliwa kama watoto wa mama mtumwa. Serikali zilihofia vurugu ya kiuchumi, kuporomoka kwa uchumi kwenye koloni na malalamiko ya wenye watumwa Uingereza walioweza kushtaki serikali mahakamani.

Uingereza ilipitisha Sheria ya Kukomesha Utumwa mnamo 1833. Wakati Sheria ya Kukomesha Utumwa ilipoanza kutumika mnamo 1834, karibu watumwa 700.000 katika Visiwa vya Karibi vya Kiingereza mara moja wakawa huru; watumwa wengine waliachiliwa miaka kadhaa baadaye. Utumwa ulifutwa katika koloni za Uholanzi mnamo 1814. Hispania ilifuta utumwa katika himaya yake mnamo 1811, isipokuwa Kuba, Puerto Rico, na Santo Domingo; Hispania ilimaliza biashara ya watumwa kwenda makoloni haya mnamo 1817, baada ya kulipwa pauni 400.000 na Uingereza. Utumwa katika Kuba uliendelea hadi 1886. Ufaransa ilikomesha utumwa katika makoloni yake mnamo 1848.

Kufuatia ukombozi wa watumwa mnamo 1833 nchini Uingereza, Waafrika wengi waliokombolewa waliwaacha mabwana zao wa zamani. Wengi hawakuwa tayari kurudi kwenye kazi hiyo. Hii ilileta matatizo ya kiuchumi kwa wamiliki wa mashamba ya miwa.

Waingereza walitafuta wafanyakazi waüya waisiodai mishahara makubwa. Wafanyakazi hao walipatikana China na baadaye zaidi kule Uhindi. Waingereza walitunga mfumo mpya wa kisheria wa kazi ya kulazimishwa, ambayo kwa njia nyingi ilifanana na utumwa wa muda. Badala ya kuwaita watumwa, wafanyakazi hao waliitwa "wafanyakazi wa mkataba" indentured labourers. Masharti ya kupata nafasi ya kazi ilikuwa kutia sahihi kwenye makataba ambako walikubali kuwa na deni kwa "gharama za safari" wakipaswa kukubali kufanya kazi kwa miaka mitano au zaidi bila haki ya kuondoka mapema. Katika kipindi hiki -ambako kutoroka kulitazamiwa kama kosa au hata jinai- mabwana walikuwa na mamlaka juu yao iliyofanana na utumwa.

Wakazi wengi wa leo kwenye visiwa vya Karibi ni wajukuu wa watumwa na wafanyakazi wa kimkataba mamilioni walioletwa katika Karibi

                                     

2.3. Mwanzo wa ukoloni Uasi wa watumwa

Mfumo wa kilimo na biashara ya watumwa ambayo iliwezesha ukuaji wake ilisababisha upinzani wa watumwa mara kwa mara katika visiwa vingi vya Karibi wakati wote wa ukoloni. Upinzani ulifanywa kwa kutoroka kutoka kwenye mashamba kabisa, na kutafuta kimbilio katika maeneo yasiyokuwa na makazi ya Wazungu. Jamii za watumwa waliotoroka, ambao walijulikana kama Maroons, waliungana pamoja katika maeneo yenye misitu minene na milima ya Antilles Kubwa na visiwa vingine vya Antilles Ndogo. Kuenea kwa mashamba na makazi ya Ulaya mara nyingi kulimaanisha kumalizika kwa jamii nyingi za Maroon, ingawa walinusurika Saint Vincent na Dominica, na katika maeneo ya milimani ya mbali ya Jamaica, Hispaniola, Guadeloupe na Cuba.

                                     

2.4. Mwanzo wa ukoloni Uasi wa watumwa wa Karibea 1522-1844

Jedwali lifuatalo linaorodhesha maasi ya watumwa ambayo yalisababisha maasi halisi:

                                     

3. Uhuru

Haiti, koloni la zamani la Ufaransa la Saint-Domingue huko Hispaniola, lilikuwa taifa la kwanza la Karibi kupata uhuru kutoka kwa nguvu za Ulaya mnamo 1804. Hii ilifuata miaka 13 ya vita ambayo ilianza kama uasi wa watumwa mnamo 1791 na ikageuka haraka kuwa Mapinduzi ya Haiti chini ya uongozi wa Toussaint Louverture, ambapo watumwa wa zamani walishinda jeshi la Ufaransa mara mbili, jeshi la Hispania, na jeshi la Uingereza, kabla ya kuwa jamhuri ya kwanza na ya zamani nyeusi duniani, na pia jamhuri ya pili kwa kongwe katika Ulimwengu wa Magharibi baada ya Marikani. Hii pia inajulikana kama kuwa pekee ya mafanikio ya uasi wa watumwa katika historia. Theluthi mbili zilizobaki za Hispaniola zilishindwa na vikosi vya Haiti mnamo 1821 na kuwa chini ya Haiti. Mnamo 1844, sehemu ya Kihispania ilipata uhuru wake kama Jamhuri ya Dominika.

Kuba na Puerto Rico zilibaki kama makoloni ya Hispania hadi Vita ya Marekani dhidi Hispania mnamo 1898. Baada ya hapo Kuba ilikuwa kwa miaka kadhaa koloni la Marekani hadi kupata uhuru wake mnamo 1902, lakini Marekani ilibaki na kituo cha Guantanamo ikaingilia katika siasa ya Kuba mara kadhaa. Mapinduzi ya Kuba ya 1959 yalileta serikali ya kikomunisti iiyovunja kila uhusiano na Marekani. Puerto Rico ikawa koloni la Marekani hadi 1917 ambako watu wake walipokea uraia wa Marekani; sasa ni eneo la pekee la Marekani. Kuna raia wanaodai uhuru, kuna pia wale wanaotaka kuwa jimbo la Marekani kamili.

Kati ya 1958 na 1962 sehemu kubwa ya Karibi iliyodhibitiwa na Uingereza ilijumuishwa kama Shirikisho jipya la West Indies katika jaribio la kuunda serikali moja huru ya baadaye - lakini ilishindikana. Makoloni yalipata uhuru wao wenyewe; Jamaika 1962, Trinidad na Tobago 1962, Barbados 1966, Bahamas 1973, Grenada 1974, Dominica 1978, Saint Lucia 1979, Saint Vincent na Grenadini 1979, Antigua na Barbuda 1981, Saint Kitts na Nevis 1983.                                     

4. Visiwa hivi sasa ambavyo si nchi za kujitegemea

Kuanzia karne ya 21 sio visiwa vyote vya Karibi vilivyoendelea kuwa nchi huru. Visiwa kadhaa vinaendelea kuwa na uhusiano wa karibu na nchi za Ulaya, au na Marekani.

Ufaransa ilibaki na makoloni kadhaa ambayo kwa sasa yote yana hali za kuwa sehemu za Ufaransa na hivyo hutazamiwa kama sehemu za Umoja wa Ulaya. Wakazi ni raia wa Ufaransa wenye haki zote za kisiasa na kijamii. Visiwa hivi ni Guadeloupe, Martinique St Martin na Saint-Barth.

Marekani inatwala Puerto Rico na Visiwa vya Virgin vya Marekani kama maeneo maalum. Wakazi ni raia kamili ya Marekani.

Ufalme wa maungano Uingereza bado una maeneo ya ngambo nje ya nchi kwenye visiwa vya Karibi ambayo ni pamoja na:

 • Bermuda
 • Visiwa vya Virgin vya Uingereza
 • Anguilla
 • Visiwa vya Cayman
 • Visiwa vya Turks na Caicos
 • Montserrat

Aruba, Curaçao, na Sint Maarten zote ni nchi za pekee ambazo bado huhesabiwa kama sehemu za "Ufalme wa Nchi za Chini" Kingdom of the Netherlands, pamoja na Uholanzi yenyewe. Nchi hizo si sehemu za Umoja wa Ulaya. Raia wa visiwa hivi wana uraia kamili wa Uholanzi wako pia raia wa Umoja wa Ulaya.

                                     
 • visiwa katika Bahari ya Karibi Pamoja na Antili Ndogo, Visiwa vya Turks na Caicos na Bahamas vinaunda visiwa vya Karibi Antili Kubwa ni hasa visiwa
 • mji mkuu wa Visiwa vya Virgin vya Uingereza katika Bahari ya Karibi Mji upo kando la hori ya bahari ya Road Harbour kenye pwani la kusini ya kisiwa. Road
 • Pedro Cays ni visiwa vinne vidogo vya bahari ya Karibi karibu na Jamaika.
 • Amerika Kusini. Inajumisha nchi za shingo ya nchi kati ya Marekani na Kolombia pamoja na visiwa vya Karibi Kwenye shingo hiyo kuna nchi zifuatazo: Belize
 • Kayimit ni visiwa pacha vya bahari ya Karibi karibu na Haiti. Kisiwa kina eneo la kilometa mraba 45 na wakazi 18, 000.
 • Thomas na mji mkuu wa Visiwa vya Virgin vya Marekani. Hii ni funguvisiwa ambayo ni sehemu ya Antili Ndogo katika Bahari ya Karibi karibu na Puerto Rico
 • Saint Vincent na Grenadini ni nchi ya visiwani ya Antili Ndogo katika bahari ya Karibi Iko kaskazini kwa Grenada na Trinidad na Tobago na kusini kwa
 • visiwa vya Karibi Denmark ilikuwa pia na maeneo madogo katika Afrika ya magharibi hasa kwa kusudi la biashara ya watumwa waliohitajika kwa ajili ya kilimo
 • Esparta ni mojawapo kati ya majimbo 23 yanayounda Venezuela peke yake ni la visiwani. Liko katika bahari ya Karibi katika visiwa vya Margarita, Coche na
 • Kiholanzi ni visiwa kadhaa katika Bahari ya Karibi kati ya Puerto Rico na pwani ya Venezuela Amerika Kusini vinavyohesabiwa kati ya visiwa vya Antili Ndogo
 • halafu Visiwa vya Kanari na Visiwa vya Madeira katika Atlantiki. Mafunguvisiwa madogo karibu na pwani ya Afrika ya Mashariki ni kama vile ya Lamu, Kilwa

Users also searched:

...

Comoro Island JamiiForums.

Kudumu kwa maisha ya wanyama wa porini ni jambo linalotuhusu ganyika na Visiwa vya Zanzibor. 2. Sentsa utalli, Lakini utajiri wa maliasili na vivutio vya utalii nchini 15.5.2.3 Juhudi za ushirikiano wa karibu zaidi kati ya Tanzania. Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya Kura Yetu. Kutumika katika kuchunguza asili na historia ya watumiaji wa majina hayo. 1: Baadhi ya Maeneo ya Karibu na Mji wa Chake Chake, Kusini Pemba. 5 Kuna makundi mengine ya watu yanayoishi katika visiwa vya Unguja na Pemba. Historia Tovuti Kuu ya Serikali. Janga hili sio tu linatishia maisha na afya ya watu bilioni 7 ulimwenguni, vituo vya hifadhi ya kimataifa na kikanda za vifaa vya kupambana na janga. ya ujenzi wa jamii ya karibu ya China Afrika ya siku zijazo kwa pamoja.


...