Back

ⓘ Sinagogi. Jina linatokana na neno la Kigiriki συναγωγή syunagoge, likimaanisha mkutano; ni tafsiri ya neno la Kiebrania בית כנסת beit knesset, yaani nyumba ya m ..
Sinagogi
                                     

ⓘ Sinagogi

Jina linatokana na neno la Kigiriki συναγωγή syunagoge, likimaanisha "mkutano"; ni tafsiri ya neno la Kiebrania בית כנסת beit knesset, yaani "nyumba ya mkutano".

Wayahudi hutumia pia neno la Kiyiddish "shul" =shule kutajia sinagogi.

                                     

1. Muundo

Chumba kikuu ni ukumbi wa sala lakini mara nyingi kipo pamoja na vyumba vya pembeni kama vile madarasa, ofisi na vinginevyo.

Ukumbi wa sala huwa na sehemu zifuatazo:

  • taa inayoendelea kuwaka muda wote;
  • mimbari ya mafundisho;
  • sanduku la Torati ni kabati au sanduku ambako hati za kuviringisha zenye mwandiko wa Biblia ya Kiebrania hutunzwa;
  • meza ya msomaji ambako hati za torati hufunguliwa na kusomwa;
  • kinara cha menorah chenye mishumaa 7 au 9.
                                     

2. Historia

Katika Israeli ya Kale kabla ya maangamizi ya Yerusalemu mwaka 587 KK inaonekana hakukuwa na sinagogi: walau halitajwi kabisa katika Agano la Kale.

Hakuna uhakika kamili lakini inaonekana ya kwamba masinagogi yalianzishwa baada ya hekalu ya Yerusalemu kubomolewa pamoja na kuanza uhamisho wa Wayahudi kwenda nchi mbalimbali.

Baada ya hekalu hilo kujengwa upya, masinagogi yaliendelea kutumiwa na Wayahudi kama nyumba ya kuabudia pia, ila si ya kutolea sadaka za altareni.

Tofauti ni kwamba masinagogi yalikuwa mengi katika Israeli na mahali pote walipoishi Wayahudi nje ya nchi hiyo, lakini kulikuwa na hekalu moja tu duniani, lile la Yerusalemu ambalo kila Myahudi, hata kama alikuwa mbali na mji huo, alipaswa kwenda kuabudu kule wakati wa sikukuu za mwaka.

Tangu kuharibiwa kwa Hekalu la Pili mwaka 70 Wayahudi wana masinagogi tu kufanyia ibada.