Back

ⓘ Waraka kwa Waebrania. Barua kwa Waebrania ni kati ya vitabu 27 vya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo. Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatak ..
Waraka kwa Waebrania
                                     

ⓘ Waraka kwa Waebrania

Barua kwa Waebrania ni kati ya vitabu 27 vya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

                                     

1. Mazingira

Miaka ya 60 B.K. Mkristo mwenye asili ya Kiyahudi na elimu ya Kiyunani, aliwaandikia Wakristo wa Kiyahudi wenzake si barua hasa, bali hotuba kamili iliyoambatanishwa na kipande cha barua.

Hali iliyosababisha uandishi ni baadhi yao kuvutiwa tena na dini yao asili na ibada zake hekaluni: kishawishi kilikuwa kikubwa hasa kwa sababu Kanisa lilikuwa bado mwanzoni, bila mahali maalumu pa kusali wala ibada za fahari.

Mwandishi aliwaonya kuwa wakimuasi Yesu hawamrudii Mungu aliye hai, aliyejifunua hasa katika Mwanae, bali wanamsulubisha tena kwa makusudi mazima na kustahili tu moto wa milele.

                                     

2. Mwandishi

Ingawa Waraka huu umehusianishwa na zile za Mtume Paulo, toka zamani ilijulikana kuwa mwandishi wake si yeye, ila mtu aliyeshirikiana naye. Kati ya wanaotajwa zaidi kuna Barnaba na Apolo.

                                     

3. Mada

Sehemu kubwa ya maandishi hayo inalinganisha Yesu Kristo na ukuhani wake katika hekalu la mbinguni upande mmoja, na ukuhani wa Agano la Kale huko Yerusalemu upande mwingine.

Hivyo mwandishi alielekeza safari ya kiroho katika imani inayofanana na ile ya watakatifu wa Agano la Kale.

Kwa kuwa lengo halikuwa la kinadharia, bali kuhimiza uaminifu, kila baada ya kuchambua ukweli fulani aliongeza mawaidha ya kufaa.

                                     

4. Ubora wa kitabu hiki

Ubora wake ni kulinganisha mambo ya kale na utimilifu wake katika Agano Jipya, pia kuthibitisha ukuu wa Kristo kama kuhani wa milele Eb 1:1-2:4; 4:11-5:10; 7:1-8:13; 10:19-11:40; 13:22-25. Hiyo inaendana na ufasaha wa lugha.

                                     

5. Marejeo

 • Heen, Erik M. and Krey, Philip D.W., eds. Ancient Christian Commentary on Scripture: Hebrews. Downers Grove, IL: Intervarsity Press, 2005.
 • Attridge, Harold W. Hebrews. Philadelphia, PA: Fortress Press, 1989.
 • Lane, William L. Hebrews 9–13. Word Biblical Commentary Vol. 47B. Dallas, TX: Word Books, 1991.
 • Guthrie, Donald The Letter to the Hebrews. Grand Rapids, MI: Wm. B. Eerdmans Publishing Co., 1983
 • Lane, William L. Hebrews 1–8. Word Biblical Commentary Vol. 47A. Dallas, TX: Word Books, 1991.
 • Koester, Craig R. "Hebrews". Anchor Bible 36. New York: Doubleday, 2001.
 • Hagen, Kenneth. Hebrews Commenting from Erasmus to Beze. Tübingen: J.C.B. Mohr Paul Siebeck, 1981.
 • Paul Ellingworth Reading through Hebrews 1–7, Listening especially for the theme of Jesus as high priest. Epworth Review 12.1 Jan. 1985: 80–88.
 • OBrien, Peter T. The Letter to the Hebrews. Pillar New Testament Commentary. Grand Rapids: Eerdmans / Nottingham: Apollos, 2010.
 • Hurst, L. D. The Epistle to the Hebrews: Its Background of Thought. Cambridge: Cambridge University Press, 1989.
 • Paul Ellingworth, The Epistle to the Hebrews. New International Greek Testament Commentary, Eerdmans, 1993
 • Hughes, P.E. A Commentary on the Epistle to the Hebrews. Grand Rapids, MI: William B. Eerdmans Publishing Company, 1977.
 • Bruce, Frederick F. The Epistle to the Hebrews. New International Commentary on the New Testament. Grand Rapids: Eerdmans, 1964. Rev Ed 1990.


                                     

6. Viungo vya nje

Ufafanuzi

 • Catholic Encyclopedia: Epistle to the Hebrews
 • Goodspeeds introductory analysis of Hebrews, 1908 at earlychristianwritings.com
 • The letter to the Hebrews in "biblical literature", Encyclopædia Britannica Online.
 • Eusebius Church History 3.3.5 includes comment by Eusebius on canonicity of Hebrews and also extensive note by Philip Schaff on topic
 • Holiness in Hebrews – Wayne G. McCown page 58
 • Encyclopædia Britannica: Hebrews, Epistle to the Archived Novemba 20, 2018 at the Wayback Machine., 1911 version
 • Eastons Bible Dictionary 1897: Epistle to the Hebrews