Back

ⓘ Zama za Mawe zilikuwa kipindi kirefu cha historia ya awali ya binadamu. Jina hilo linatokana na kwamba wakati huo watu walitumia vifaa vya mawe kwa shughuli zao ..
Zama za Mawe
                                     

ⓘ Zama za Mawe

Zama za Mawe zilikuwa kipindi kirefu cha historia ya awali ya binadamu. Jina hilo linatokana na kwamba wakati huo watu walitumia vifaa vya mawe kwa shughuli zao za kila siku.

                                     

1. Utamaduni wa watu mwanzoni mwa zama za mawe

Mwanzoni watu walikuwa wawindaji-wakusanyaji, yaani walidumisha maisha yao kwa kukusanya matunda, mizizi na kuwinda wanyama.

Kwa umbile na akili yake binadamu ana uwezo wa kuwinda wanyama wakubwa kama chakula na kutumia ngozi yao kama mavazi ya kujikinga dhidi ya baridi.

Lakini meno na makucha yake hayafai kupasua ngozi ya mnyama mkubwa au kukata nyama yake vipande-vipande akitaka kubeba windo hadi mahali penye familia yake. Vilevile makucha hayafai sana kuchimba mizizi kwa chakula.

Hapo binadamu aliweza kutumia vitu vinavyopatikana kiasili katika mazingira: jiwe lenye kona kali, tawi la mti lenye ncha kali pamoja na vipande vya mifupa. Hivyo vyote vilisaidia shughuli za kuchimba, kupasua na kukata.

Kuna mabaki mengi ya mawe yaliyochongwa kwa matumizi kama vifaa na mabaki hayo yamekuwa msingi wa jina "zama za mawe". Vifaa hivyo na mabadiliko yake vinaonyesha maendeleo katika maisha ya binadamu na kuongezeka kwa uwezo wake wa kupambana na mazingira yake.

Kwa hiyo ni kipindi cha matumizi ya mawe yaliyochongwa kuwa vifaa baada ya kipindi ambako watu walitumia fimbo tu au mawe katika hali asilia na kabla ya kipindi ambapo watu walielewa namna ya kutumia metali.

                                     

2. Vipindi vya zama za mawe

Wataalamu wa akiolojia wametambua ya kwamba vifaa vya mawe vinaonyesha tabia tofautitofauti.

 • Kuna pia vifaa vya mawe vinavyoonyesha maendeleo zaidi; vilifanyiwa kazi kwa siku kadhaa kiangalifu ili kunyoshwa, kungarishwa na kutobolewa kwa kuweka pini.
 • Kuna vifaa sahili sana kama jiwe lililogongwa mara moja ili kipande kivunjike na ncha kali ipatikane.

Kutokana na tofauti kubwa katika hali ya vifaa vya mawe wataalamu wanaona ya kwamba wanaonyesha historia ndefu ya maendeleo ya teknolojia ya kushughulikia jiwe ambako watu walianza kwa vifaa sahili na kuendelea kujifunza zaidi na kuboresha matokeo ya juhudi zao.

Kwa hiyo wataalamu wengi wanatofautisha:

 • Zama za mawe za kati pia: Zama za kati za mawe
 • Zama za mawe za kale pia: Zama za mwanzo za mawe
 • Zama za mawe za mwisho pia: Zama za mwisho za mawe

Si tofauti katika ubora wa vifaa pekee, lakini kuna pia dalili nyingine zinazoonyesha ya kwamba watu walibadilisha maisha yao, namna ya kujipatia chakula na makazi.

Kila mtu aliweza kugonga jiwe dhidi ya jiwe hadi ncha kali ilipatikana. Lakini mashoka ya mawe yaliyohitaji siku za kazi makinifu yanaonyesha kuwepo kwa jamii iliyokuwa na mafundi wa pekee walioweza kunyosha ufundi wao wakilishwa na wengine ni pia dalili ya biashara iliyofanywa hasa tukikuta vifaa vya jiwe fulani katika maeneo ambako jiwe hili halipatikani kiasili.

Pamoja na matokeo mengine ya utafiti wa akolojia, kama vile mabaki ya makaburi, vyombo vya ufinyanzi, nyumba na vifaa vingine, wataalamu waliweza kupata picha ya undani zaidi kuhusu maisha na jamii ya watu wa zamani zile.

                                     

3.1. Vifaa vya mawe Zama za mawe ya kale

Vifaa vya kwanza vilikuwa mawe yaliyokatwa upande mmoja ili kuwa na kona kali moja. Hatuwezi kujua kwa uhakika tukiona jiwe la aina hii kama ilikuwa tokeo la mgongano wa mawe katika mkondo wa maji mtoni au kutokana na kuanguka kwa jiwe kutoka mlimani au kama jiwe limepigwa kwa kusudi kwa jiwe lingine kwa shabaha ya kupata kona kali. Lakini mawe haya yalifaa kutumiwa kwa kukata pia si vigumu kuvitengeneza.

Mifano ya kale kabisa ya mawe yaliyogongwa kwa mawe mengine kwa kusudi la kupata kona kali zimepatikana katika eneo la ziwa Turkana leo nchini Kenya yalitegenezwa miaka milioni 3.3 iliyopita.

Ngazi iliyofuata ni mawe yaliyofanyiwa kazi zaidi hadi kuwa "shoka la mkononi". Hapo jiwe la kufaa lilipigwa na kupunguzwa pande zote mbili hadi kuwa na bapa pande mbili. Sehemu ya juu ilibaki bila ukali kwa kuishikilia mkononi. Kuna mahali ambako mabaki mengi ya mashoka haya ya mkononi yamepatikana katika hali mbalimbali: mawe yaliyopigwa kiasi, mawe yaliyovunjika vibaya na kutupwa, vipande vidogo vilivyopasuliwa wakati wa kuipa shoka umbo lake na kadhalika. Mahali pale panatazamwa kama karakana au viwanda vya kutengeneza vifaa vya mawe. Mahali mashuhuri katika Afrika ya Mashariki ni bonde la Isimila karibu na Iringa, Tanzania ya leo.                                     

3.2. Vifaa vya mawe Zama za mawe ya kati

Kipindi hiki kinatazamwa kilianza miaka 300.000 iliyopita na kudumu hadi miaka 25.000 - 50.000 iliyopita.

Kipindi hiki kinaonyesha maendeleo ya teknolojia. Watu walianza kutumia pia vipande vidogo vikali vilivyopatikana wakati wa kupunguza jiwe. Vibanzi vikali vya mawe vilifungwa sasa kwenye pini ya ubao kwa gundi la miti. Kwa njia hii vifaa kama kisu, chusa au mundu vilipatikana.

                                     

4. Matatizo ya lugha ya "zama za mawe"

Zama za mawe zilikuwa vipindi virefu sana vya miaka elfu nyingi. Wataalamu wamegawanya zama hizo katika vipindi mbalimbali kama Zama za mawe za kale na Zama za mawe za kati. Tofauti hizo zinaonekana kuwa na msingi, lakini wataalamu wa siku hizi wanaona ya kwamba mgawanyo huu ulitazama zaidi historia ya Ulaya isiyolingana na historia ya sehemu nyingine za dunia.

Tatizo kuu ni kwamba ni kipindi cha teknolojia bila kuangalia pande nyingine za maendeleo ya kibinadamu.

Kwa mfano chuma hakikutumiwa huko Amerika hadi karne ya 16 na huko Pasifiki hadi karne ya 17. Hata hivyo jamii za Amerika kama Azteki au Wainka walikuwa na teknolojia nyingine mbalimbali na waliweza kudumisha miji mikubwa kushinda miji ya Ulaya ya wakati ule.

Basi, lugha ya "zama za mawe" imekuwa kawaida duniani na wataalamu wanaendelea kuitumia wakijua kasoro zake kwa sababu hadi sasa hakuna mawazo ya kufaa zaidi.

                                     

5. Viungo vya nje

 • PanAfrican Archaeological Association. Iliwekwa mnamo 28 February 2011.
 • Society of Africanist Archaeologists. Iliwekwa mnamo 3 March 2011.
 • The ASA. Association of Social Anthropologists of the UK and Commonwealth.
 • Kowalski, D.R. Stone Age Habitats. AerobiologicalEngineering.com. Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-03-17. Iliwekwa mnamo 22 February 2011.
 • Kowalski, D.R. Stone Age Hand-axes. AerobiologicalEngineering.com. Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-03-17. Iliwekwa mnamo 22 February 2011.
 • Giusepi, Robert A. 2000. The Stone Age. History World International. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-02-22. Iliwekwa mnamo 22 February 2011.
                                     
 • tangu zama za mawe Upanga, pinde na mshale pamoja na mikuki zilikuwa silaha kwa milenia nyingi lakini ziliboreshwa tena na tena. Tangu nyakati za kati
 • vilikuwa vifaa vya mawe yaliyokatwa kuwa visu, shoka au nyundo. Tangu zama za mawe miamba ilitumiwa na binadamu kama zana. Wakati wa zama za mawe watu walikuwa
 • linaunda jamhuri ya Kijamaa ya Vietnam. Nchi ilikaliwa na watu tangu Zama za Mawe Vietnam ilitawaliwa kwa karne kadhaa kutoka China kuanzia karne ya 2
 • maarufu sana, na kama vile migodi mingine ya majani, ni asili ya zama za mwisho za mawe ca 4000 - 3000 BC Miamba mingine migumu iliyopigwa au iliyokusanywa
 • cha kuyeyuka ni 1, 083 C Ni kati ya metali za kwanza wanadamu walizotumia baada ya kutoka katika zama za mawe Si metali ngumu sana, hivyo ilikuwa nyepesi
 • mazao mengine. Mundu kama zana ya kilimo inajulikana tangu zama za mawe Katika nchi nyingi za dunia haitumiwi tena sana kwa sababu nafasi yake imechukuliwa
 • za mapango lakini tunakosa maelezo jinsi yanavyopatikana tangu watu waanze kuandika kumbukumbu. Kati ya vipindi vya historia ya awali ni zama za mawe
 • kidemokrasia ya shirikisho la Nepal. Vyombo vya watu waliokuwa wakiishi katika zama za mawe zilipatikana katika bonde la Kathmandu kuonyesha kwamba kumekuwa na watu
 • linaunda jamhuri ya Azerbaijan. Azerbaijan ina historia ndefu kuanzia Zama za Mawe Kuanzia karne ya 9 KK ilikaliwa na Washitia, halafu Wamedi, wote wa
 • makaa ya mawe ili kuweza kutembea. Meli za mizigo za kisasa zinaweza kubeba mizigo mingi na mizito kama vile magari, mashine mbalimbali za kazi na kusafirisha
 • wageni wametazama kwa watu wa Bushmen kwa dalili za jinsi wanadamu walivyoweza kuishi katika Zama za Mawe halafu Waethiopia. Mwaka 2000 idadi ya Wasandawe

Users also searched:

...

HALI YA UCHUMI NA MAENDELEO YA JAMII MKOA WA DODOMA.

Kuna utamaduni wa urithi ambao ni pamoja na masalia ya zamadamu, masalia ya akiolojia kama zama za mawe na zama za chuma za. Dk. Shein adhihirisha kwa vitendo dhamira ya SMZ Ikulu Zanzibar. Teknolojia imetoka mbali,kipindi cha kupekesha moto,zama zile za uwimbombo na ulindi. Zama zimebadilika,kutoka zama za mawe za. Utalii kiutamaduni mikoani unaweza kuondoa umaskini IPPMEDIA. Hakika andiko lilitimia hazifai kuta za mawe, unapomtuma wako mjumbe nchini Tanzania, Baba Timanywa alifunga zama za Papa Paulo VI,.


...