Back

ⓘ Mtaguso wa kwanza wa Vatikano, unatazamwa na Kanisa Katoliki kama Mtaguso Mkuu wa ishirini katika historia yake. Uliitishwa rasmi na Papa Pius IX 1846-1878 mnam ..
Mtaguso wa kwanza wa Vatikano
                                     

ⓘ Mtaguso wa kwanza wa Vatikano

Mtaguso wa kwanza wa Vatikano, unatazamwa na Kanisa Katoliki kama Mtaguso Mkuu wa ishirini katika historia yake.

Uliitishwa rasmi na Papa Pius IX 1846-1878 mnamo 29 Juni 1867 na vikao vyake viliendelea katika Basilika la Mt. Petro huko Vatikano mjini Roma kuanzia tarehe 8 Desemba 1869 hadi vilipokatika mnamo 1870 kutokana na jeshi la Italia kuteka Roma tarehe 20 Septemba.

Walishiriki maaskofu na mapadri 774 kati ya 1050 wenye haki ya kuhudhuria, ambao kwa mara ya kwanza walitokea mabara yote. Pia ilikuwa mara ya kwanza ya kutokuwepo wawakilishi wa serikali. Kumbe wajumbe wa Waorthodoksi na wa Waprotestanti walialikwa pia, lakini hawakufika.

Tarehe 24 Aprili 1870, baada ya majadiliano mengi, ilipitishwa hati "Dei Filius" juu ya Mungu, ufunuo, imani, na uhusiano kati ya imani na akili.

Ingawa lengo halikuwa hilo, tokeo kuu la kazi ya mtaguso huo ni tangazo la dogma ya Papa kuwa na karama ya kutokosea katika mafundisho ya imani na maadili anayoyatoa ili yadumu moja kwa moja pale anapotimiza masharti fulani kwa kifupi: akisema "ex cathedra", yaani "kutoka ukulu.

Dogma hiyo iliimarisha mamlaka ya Papa na umoja wa Kanisa dhidi ya maelekeo ya kitaifa ambayo yalitawala karne zilizotangulia yakisababisha matatizo mengi.

                                     

1. Viungo vya nje

 • Hati za Mtaguso huo kwa Kiingereza.
 • Kitabu THE TRUE AND THE FALSE INFALLIBILITY OF THE POPES Archived Septemba 27, 2006 at the Wayback Machine. *Kuhusu Askofu Joseph Fessler 1813-1872, katibu mkuu wa mtaguso.
                                     
 • Mtaguso wa Yerusalemu au Mtaguso wa mitume ni jina linalotumika kwa mkutano uliofanyika mwaka 49 au 50 ili kuondoa tofauti za misimamo kati ya Wakristo
 • wake. Halafu papa alikusudia kuendeleza juhudi za urekebisho za Mtaguso wa kwanza wa Laterano. Hivyo zikapitishwa kanuni 30, ambazo nyingi kati yake zilikuwa
 • Fundisho hilo, lililosisitizwa na Mtaguso wa pili wa Vatikano linatekelezwa hasa maaskofu wanapokutana katika Mtaguso mkuu, lakini pia katika Sinodi ya
 • II kufuatana na Mtaguso wa pili wa Vatikano Kanuni zote za Mkusanyo huo katika Tovuti ya Vatikani Kamati ya Papa kwa Ufafanuzi Rasmi wa Sheria za Kanisa
 • Christus Dominus ni maneno mawili ya kwanza ya hati iliyotolewa kwa Kilatini na Mtaguso wa pili wa Vatikano kuhusu kazi ya maaskofu. Maneno hayo yana maana
 • mchanganyiko wa watu ambao siku hizi unaongezeka mahali pengi, Mtaguso wa pili wa Vatikano uliona haja ya kutoa tamko juu ya uhusiano wa Kanisa Katoliki
 • kuonyesha nia yake ya kuendeleza kazi yao, hasa Mtaguso wa pili wa Vatikano Ilikuwa mara ya kwanza kwa Papa kuchagua jina dabo. Ingawa muda haukumruhusu
 • Hati hiyo ilitolewa na Mtaguso wa pili wa Vatikano tarehe 7 - 12 - 1965, siku ya mwisho kabla ya kufunga, kwa kura 2390 dhidi ya 4 tu. Jina lake kwa Kilatini
 • ileile 28 - 10 - 1965 ambayo Mtaguso wa pili wa Vatikano uliyotoa hati kuhusu uchungaji wa maaskofu na kuhusu urekebisho wa watawa, ilitolewa nyingine tena

Users also searched:

...

UMOJA NA MAPENDO The Catholic Diocese of Singida.

Wahenga wasimulia ujio wa Wamisonari wa kwanza Singida. Hati ya Mtaguso wa Vatikano II inayozungumzia Malezi ya Waseminari Optatam. Parokia za mwanzo kabla ya singida kuwa jimbo The Catholic. Wakati wa vita ya kwanza ya dunia, Padre Roncali alihudumu kama na kuitisha Mtaguso Mkuu wa Vatikano II, mnamo tarehe 11 10 1962.


...