Back

ⓘ Mtaguso wa pili wa Lyon. Mtaguso wa pili kufanyika Lyon Ufaransa ulikusudiwa hasa kurudisha umoja kamili kati ya Wakatoliki na Waorthodoksi, uliotafutwa katika ..




Mtaguso wa pili wa Lyon
                                     

ⓘ Mtaguso wa pili wa Lyon

Mtaguso wa pili kufanyika Lyon Ufaransa ulikusudiwa hasa kurudisha umoja kamili kati ya Wakatoliki na Waorthodoksi, uliotafutwa katika karne ya 13 yote.

Mnamo Februari 1274, katika ikulu ya Konstantinopoli, kaisari Mikaeli VIII ilifaulu kufanya maaskofu wengi wakiri ungamo la imani lililodaiwa na Papa Klementi IV 1265-1268.

Ndipo Papa Gregori X 1271-1276 alipoitisha mtaguso huko Lyon, ambao uhudhuriwe na wawakilishi wa Waorthodoksi ili kukamilisha umoja.

                                     

1. Kazi na maamuzi ya mtaguso

Papa Gregori X alifungua mtaguso tarehe 7 Mei 1274 akitangaza tena malengo yake matatu: kusaidia Wakristo wa Nchi takatifu, kuungana tena na Waorthodoksi na kurekebisha maadili ndani ya Kanisa.

Vilifuata vikao viwili tarehe 18 Mei na 4 Juni. Halafu tarehe 24 Juni ulifika na kupokewa kwa shangwe ujumbe kutoka Ugiriki, ukiundwa na maaskofu 2 na katibu wa kaisari.

Tarehe 6 Julai kilifanyika kikao cha nne kwa ajili ya muungano na hatimaye tarehe 16 Julai kile cha mwisho kilichopitisha hati mbalimbali za urekebisho. Kesho yake mtaguso ulifungwa.

                                     

2. Mapokezi ya mtaguso

Muungano haukuweza kudumu, kwa sababu, alivyoandika Papa Paulo VI 1963-1978 tarehe 19 Oktoba 1974, ulifanyika "bila ya kulipatia Kanisa la Kigiriki nafasi ya kutokeza kwa hiari mtazamo wake kuhusu jambo hilo. Wakristo wa Kilatini ndio waliotunga hati na matamko kufuatana na mafundisho juu ya Kanisa yaliyofafanuliwa na kupangwa magharibi".

Mikaeli VIII alijaribu kulazimisha raia zake wapokee mambo wasiyoyakubali kwa moyo, hata akatumia nguvu kuwadhulumu waliokataa; akilaumiwa na watu wa Roma kwa kushindwa kufanikisha muungano, akaja kutengwa na Kanisa. Alipokufa 1282, mwanae Androniko II aliyemrithi, alifuta maamuzi ya baba yake kwa ajili ya muungano.

Vilevile mipango kwa ajili ya vita vya msalaba haikutekelezwa, na hatimaye 1291 Waturuki waliteka Akri, mji wa mwisho kubaki mikononi mwa Wakristo huko Mashariki ya Kati.

Maamuzi mengine yalihusu utaratibu mpya wa kumchagua Papa kwa lengo la kuzuia uchelewaji uliojitokeza hapo nyuma, na katazo la mashirika mapya ya kitawa.

                                     
 • linatolewa na Papa au Mtaguso Mpaka sasa, katika miaka karibu 2000 ya historia ya Kanisa wanaume 32 na wanawake 4 tu wamepewa heshima hiyo. Wa kwanza kutangazwa
 • yalivyokuwa mwaka 1962. Mabadiliko ya liturujia yaliyofanywa baada ya Mtaguso wa pili wa Vatikano 1962 - 1965 baadhi yakiwa halali na baadhi kinyume cha sheria
 • kuzingatia zaidi ushahidi wa historia kama ulivyoagiza Mtaguso wa pili wa Vatikano Toleo hilo linaorodhesha watu 7, 000 hivi. Watakatifu wa Agano la Kale Orodha
 • aliitisha mtaguso mkuu wa kwanza uliofanyika mwaka 325 huko Nisea. Mtaguso huo ulitunga kanuni ya imani iliyokiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu kwa maana
 • haraka haikusaidia kuzifanikisha, kwa mfano katika Mtaguso wa pili wa Lyon 1274 na katika Mtaguso wa Firenze 1431 - 1449 Njia ya taratibu iliyoshikwa
 • ya viongozi wa Kanisa hivyo waliwasaidia wasikamatwe. Uzushi wa aina nyingine ulianza muda mfupi baadaye karne XI hiyohiyo huko Lyon Ufaransa Kusini
 • akiwa askofu wa Albano Laziale, kwa agizo lake aliandaa kwa bidii Mtaguso wa pili wa Lyon ulioanza mwaka 1274 hasa kwa lengo la kurudisha umoja kati ya Wakatoliki
 • Verbe - Incarné et du Saint - Sacrament Lyon Chez Pierre Guillimin, 1662 pp. 28 29. Cf. later edition published at Lyon Chez Briday, Libraire, 1962 pp. 22 24
 • kulenga umoja na madhehebu mengine, bali linafuata njia za ekumeni. Mtaguso wa pili wa Vatikano uliyazungumzia Makanisa Katoliki ya Mashariki na kuyatolea
 • Missale plenum ilienea kote kati ya karne XIII na ile ya XV. Baada ya Mtaguso wa pili wa Vatikano, masomo yaliondolewa katika Misale na kurudishwa katika vitabu
 • ya Mtaguso wa pili wa Vatikano liturujia hiyo imeshughulikiwa sana na wachungaji na wataalamu mbalimbali hata kupata uhai mpya. Ingawa Wakatoliki wa maeneo

Users also searched:

...

Maaskofu Katoliki watoa waraka mzito Mwananchi.

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania TEC limetoa waraka wa Mtaguso wa Pili wa Vatican, uliotoa maelekezo kuhusu ufalme wa Mungu. Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate Like. Kwanza ni huo mtaguso wa awali ambao nimesema baadhi ya wataalamu wa mambo ya kanisa hawautambui. Mtaguso wa Lyon II 1274. FAHAMU MAANA YA MTAGUSO Radio Maria Tanzania. Mtaguso ni mkutano wa viongozi wa Kanisa hasa Baba Mtakatifu, Makardinali, ma Askofu karibuni ulikuwa Mtaguso wa pili wa Vatikano uliofanyika Roma kati ya 1962 na 1965 na Mtaguso wa kwanza wa Lyon 1245 14.


...