Back

ⓘ Mtaguso wa kwanza wa Nisea ndio mtaguso wa kwanza kuitwa mtaguso wa kiekumeni, yaani mtaguso wa dunia yote au mtaguso mkuu. Ndiyo sababu inashika nafasi ya peke ..
Mtaguso wa kwanza wa Nisea
                                     

ⓘ Mtaguso wa kwanza wa Nisea

Mtaguso wa kwanza wa Nisea ndio mtaguso wa kwanza kuitwa mtaguso wa kiekumeni, yaani mtaguso wa dunia yote au mtaguso mkuu. Ndiyo sababu inashika nafasi ya pekee kati ya mitaguso yote.

Uliitishwa na kusimamiwa na kaisari Konstantino Mkuu, aliyehofia mabishano kati ya raia wake Wakristo kuhusu Yesu Kristo, ambayo yalihatarisha umoja na usalama wa Dola la Roma lililoanza kuelekea kusambaratika. Yeye aliwaalika maaskofu wote wa dola, waliokuwa kama 1000 mashariki na kama 800 magharibi. Washiriki walitokea hata nje ya dola hilo, kama vile Persia na Armenia.

Katika hali hiyo mtaguso ulianza tarehe 20 Mei 325; washiriki walikuwa kama 318, wengi wao wakitokea upande wa mashariki wa dola hilo. Upande wa magharibi uliwakilishwa na watu 4 kutoka Ulaya na 1 kutoka Afrika. Papa Silvesta I 314-335 aliwakilishwa na mapadri wawili.

Asili ya mabishano ilitokea katika Kanisa la Aleksandria Misri, ambapo kasisi Arios alikuwa amekanusha umungu wa Yesu, na hivyo alihukumiwa na Sinodi ya Aleksandria ya mwaka 321, iliyoitishwa na askofu Aleksanda wa Aleksandria. Hata hivyo Arios hakuacha mafundisho yake, akakimbilia Palestina kwa rafiki yake Eusebio wa Nikomedia.

Basi, mtaguso ulikiri karibu kwa kauli moja kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu kwa maana ana ousìa yaani dhati ileile ya Kimungu aliyonayo Baba. Ndiyo kiini cha Kanuni ya imani ya Nisea iliyopitishwa na mtaguso.

Uamuzi mwingine wa mtaguso ulikuwa kupanga siku ya Pasaka, sherehe kuu ya Kanisa, iwe Jumapili inayofuata mbalamwezi ya kwanza ya majira ya kuchipua, tofauti na kalenda ya Kiyahudi. Pia zilitungwa kanuni 20 kuratibu mambo mbalimbali.

Mtaguso ulipomalizika tarehe 25 Julai 325, Konstantino alifikiri uamuzi juu ya dogma utamaliza mabishano, lakini haikuwa hivyo, kwa sababu Wagiriki wengi, ingawa hawakukubaliana na Arios, hawakuridhika na msamiati uliotumika kuelezea uhusiano wa Baba na Mwana.

                                     

1. Viungo vya nje

 • Mtaguso wa kwanza wa Nisea katika Catholic Encyclopedia
 • Atanasi wa Aleksandria, Utetezi wa Tamko la Nisea ; Atanasi wa Aleksandria, Barua ya Sinodi kwa watu wa Afrika
 • Eusebio wa Kaisarea, Eusebio wa Kaisarea, Barua kwa watu wa jimbo lake kuhusu Mtaguso wa kwanza wa Nisea Account of the Council of Nicea; Maisha ya mwenye heri kaisari Konstantino, kitabu III, sura VI-XXI zinahusu Mtaguso wa kwanza wa Nisea
 • Eustazio wa Antiokia, Barua iliyorekodiwa katika Historia ya Kanisa iliyoandikwa na Theodoreto 1.7
 • Hati zote za mtaguso katika lugha mbalimbali
                                     
 • Mtaguso wa Yerusalemu au Mtaguso wa mitume ni jina linalotumika kwa mkutano uliofanyika mwaka 49 au 50 ili kuondoa tofauti za misimamo kati ya Wakristo
 • wake. Halafu papa alikusudia kuendeleza juhudi za urekebisho za Mtaguso wa kwanza wa Laterano. Hivyo zikapitishwa kanuni 30, ambazo nyingi kati yake zilikuwa
 • Mtaguso wa Trento uliofanyika kwa kwikwi kuanzia mwaka 1545 hadi 1563 unahesabiwa na Kanisa Katoliki kuwa mtaguso mkuu wa kumi na tisa. Miaka hiyo maaskofu
 • Konstantino I aitishe Mtaguso wa kwanza wa Nisea mwaka 325. Huo mtaguso mkuu wa kwanza uliokusanya maaskofu wengi hasa wa mashariki, ulikataa hoja zake
 • alishughulikia maskini na kuwajengea hospitali kama ilivyoagizwa na Mtaguso wa kwanza wa Nisea Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu
 • kiekumeni ya kwanza Mtaguso wa kwanza wa Nisea na Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli ilitungwa ikapanuliwa kanuni ya imani ya Nisea - Konstantinopoli
 • Kisha kuachiliwa alishiriki mtaguso wa kwanza wa Nisea Rafiki mwaminifu wa Atanasi Mkuu, alimtetea kwa ushujaa katika mtaguso wa Tiro 335 na kwa ajili
 • Imani ya Nisea Konstantinopoli, iliyotungwa mwaka 325 katika Mtaguso wa kwanza wa Nisea na kukamilishwa mwaka 381 katika Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli
 • ya wahusika muhimu wa Mtaguso wa kwanza wa Nisea 325 na wanasema aliongozana na Atanasi wa Aleksandria kushiriki Sinodi ya kwanza ya Turo 335 Kabla

Users also searched:

...

Papa Francis afanya marekebisho ya Sheria za Kanisa Katoliki.

Kanisa Katoliki likiwa la zamani Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki Konstantino aliitisha huko Nisea mtaguso mkuu wa kwanza wa maaskofu wote ili Mbele ya changamoto hizo, Mtaguso wa pili wa Vatikano. Mtaguso wa Kwanza wa Nicea wa Mwaka 325 ndio uliamua kwamba Pasaka itasherehekewa Jumapili ya kwanza baada ya mwezi mpevu wa.


...