Back

ⓘ Mtaguso wa Efeso unahesabiwa na Wakristo walio wengi kama mtaguso mkuu wa tatu. Ulifanyika Efeso katika mkoa wa Asia Ndogo, kwa amri ya kaisari Theodosius II; P ..




Mtaguso wa Efeso
                                     

ⓘ Mtaguso wa Efeso

Mtaguso wa Efeso unahesabiwa na Wakristo walio wengi kama mtaguso mkuu wa tatu. Ulifanyika Efeso katika mkoa wa Asia Ndogo, kwa amri ya kaisari Theodosius II; Papa Selestini I alimteua Sirili wa Aleksandria kuuendesha; washiriki walikuwa zaidi ya 150 na kujadili vikali hasa uzushi wa Nestori wa Konstantinopoli.

                                     

1. Historia

Patriarki Nestori alikuwa anasisitiza ubinadamu wa Yesu Kristo kuliko umungu wake, akisema Bikira Maria alimzaa mtu Yesu, si Mungu, wala si Neno wa Mungu aliyehifadhiwa ndani ya nafsi ya Kristo kama hekaluni. Kwa hiyo Kristo alikuwa Theophoros, yaani "mbeba Mungu", na Maria Christotokos, "Mama wa Kristo" si Theotokos, "Mama wa Mungu".

Mtaguso huo ulilaani haraka mafundisho hayo ukikiri kwamba nafsi ya Yesu Kristo ni moja tu, ile ya milele ya Mwana wa Mungu, na kwamba nafsi hiyo ilitwaa ubinadamu kamili wenye mwili na roho. Hivyo Maria ni Theotokos kwa kuwa alimzaa Mungu kama binadamu.

Wajumbe wa Papa walipofika walithibitisha uamuzi huo, lakini maaskofu kutoka Antiokia hawakuridhika, na uzushi huo uliendelea Mesopotami na kuenea hata Asia mashariki.

Mtaguso ulitangaza kuwa Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli ni kamili ukakataza isibadilishwe kwa namna yoyote.

Pia ulilaani Upelaji, uzushi kutoka Ulaya magharibi kuhusu uwezo wa binadamu kutenda mema bila ya kusaidiwa na neema ya Mungu.

                                     
 • Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli ndio wa pili katika orodha ya mitaguso ya kiekumene ya Kanisa wakati wa mababu wake. Uliitishwa na kaisari Theodosius
 • Mtaguso wa nne wa Laterano 1215 unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na mbili. Uliitishwa na Papa Inosenti III 1198 - 1216 kama
 • Kiorthodoksi kutoka Dola la Bizanti na askofu mkuu wa Efeso Alipata umaarufu kwa kushiriki katika Mtaguso wa Ferrara - Florence 1438 1439 na kushika msimamo
 • Mtaguso wa Vienne 1311 - 1312 unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na tano. Mtaguso huu ulifanyika Vienne Ufaransa baada ya mashindano
 • Mtaguso wa pili wa Konstantinopoli uliitishwa na kaisari Justiniani I mwaka 553 kwa lengo la kupatanisha tena na Kanisa Katoliki Wakristo wote wa Misri
 • Mtaguso wa Trento uliofanyika kwa kwikwi kuanzia mwaka 1545 hadi 1563 unahesabiwa na Kanisa Katoliki kuwa mtaguso mkuu wa kumi na tisa. Miaka hiyo maaskofu
 • mengine. 1. Mtaguso wa kwanza wa Nikea mwaka 325 2. Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli 381 3. Mtaguso wa Efeso 431 4. Mtaguso wa Kalsedonia 451
 • Mtaguso wa tatu wa Konstantinopoli unahesabiwa na Wakristo wengi kuwa wa sita kati ya Mitaguso ya kiekumene. Uliitishwa tarehe 7 Novemba 680 ukafungwa
 • Mtaguso wa kwanza wa Laterano unahesabiwa na Kanisa Katoliki mtaguso mkuu wa tisa katika historia yake, wa kwanza kufanyika Magharibi. Ulianza tarehe 18
 • Mtaguso wa Yerusalemu au Mtaguso wa mitume ni jina linalotumika kwa mkutano uliofanyika mwaka 49 au 50 ili kuondoa tofauti za misimamo kati ya Wakristo
 • Mtaguso wa nne wa Konstantinopoli ni jina linalotumiwa na Wakristo kwa namna tofauti, kadiri wanavyokubali au kukataa uhalali na uekumeni wa mitaguso fulanifulani

Users also searched:

...

FAHAMU MAANA YA MTAGUSO Radio Maria Tanzania.

Unajua biblia imekamilika mwaka 300AD chini ya mtaguso wa Efeso.hahahaha.​. Kama hujui historia kaa kimya utaja aibika Nikisema Biblia. Usichojua kuhusu makanisa ya kiroho Page 11 JamiiForums. Mtaguso ni mkutano wa viongozi wa Kanisa hasa Baba Mtakatifu, Makardinali, ma Askofu pamoja na Wakristo Mtaguso wa Efeso 431 4.


...