Back

ⓘ Mtaguso wa Kalsedonia unahesabiwa na Wakristo wengi kuwa wa nne kati ya mitaguso ya kiekumene katika historia ya Kanisa. Ulifanyika Kalsedonia leo katika nchi y ..
Mtaguso wa Kalsedonia
                                     

ⓘ Mtaguso wa Kalsedonia

Mtaguso wa Kalsedonia unahesabiwa na Wakristo wengi kuwa wa nne kati ya mitaguso ya kiekumene katika historia ya Kanisa.

Ulifanyika Kalsedonia leo katika nchi ya Uturuki mwaka 451.

                                     

1. Historia

Mtaguso huo uliitishwa na Kaisari Marcianus wa Dola la Roma Mashariki pamoja na mke wake Pulkeria wa Bizanti miaka 20 baada ya Mtaguso wa Efeso.

Hao waliona haja ya kudumisha umoja wa Wakristo, uliokuwa msingi wa uimara wa dola hilo, hasa wakati huo ambapo makabila yasiyo na ustaarabu kutoka Asia yalikuwa yanajaribu kuteka Ulaya.

Umoja huo uliingia hatari ya kuvunjika kutokana na uamuzi wa mtaguso mkuu wa Efeso kuhusu imani sahihi juu ya Yesu Kristo kutoeleweka kwa namna moja.

Hasa baadhi ya walioshinda mtaguso huo walionekana kusisitiza mno umungu wake hata kutia shaka kama wanaamini sawasawa ubinadamu wake pia.

Vikao vilianza tarehe 8 Oktoba 451 vikiwa na washiriki zaidi ya 350: mara nyingi inatajwa idadi ya 600 hivi. Hatimaye mafundisho ya Eutike na Dioskoro wa Aleksandria yalilaaniwa.

Ufanisi wa mtaguso ulichangiwa na msimamo wa kaisari Valentiniano III wa Dola la Roma Magharibi, binamu wa Pulkeria. Kaisari huyo alimuunga mkono Papa Leo I 440-461 aliyekuwa ametoa msimamo wake na wa Kanisa la Roma tangu mwaka 449 katika Tomus ad Flavianum, yaani Waraka kwa Flaviano, Patriarki wa Konstantinopoli aliyeuawa na wafuasi wa Eutike.

Ingawa msimamo huo wa kati ulikubaliwa na wengi, wengine waliuona ni kinyume cha uamuzi wa Efeso, hivyo walishikilia sana mtazamo huo hata walipodhulumiwa na serikali. Ndiyo asili ya farakano la Misri, Syria, Armenia n.k. linalodumu hata leo.

Mtaguso huo ulitunga pia kanuni mbalimbali, kama vile kwa kumpatia Patriarki wa Konstantinopoli nafasi ya pili kati ya maaskofu wote.

                                     

2. Marejeo

 • R.V. Sellers, Two Ancient Christologies, London 1940
 • The Ecclesiastical History of Evagrius: A History of the Church from AD 431 to AD 594, transl. Edward Walford, 1846.
 • Charles Joseph Hefele, A History of the Councils of the Church from the Original Documents. 5 voll. in part. vol. III Edinburgh 1883
 • R.V. Sellers, The Council of Chalcedon: A Historical and Doctrinal Survey, London 1961
 • John Meyendorff, Christ in Eastern Christian Thought, Washington D.C. 1969
                                     
 • Mtaguso wa pili wa Nisea uliitishwa na malkia Irene wa Bizanti mwaka 787, ili kujadili matumizi ya picha takatifu na sanamu katika Ukristo, kutokana na
 • Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli ndio wa pili katika orodha ya mitaguso ya kiekumene ya Kanisa wakati wa mababu wake. Uliitishwa na kaisari Theodosius
 • Mtaguso wa nne wa Laterano 1215 unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na mbili. Uliitishwa na Papa Inosenti III 1198 - 1216 kama
 • Mtaguso wa Vienne 1311 - 1312 unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na tano. Mtaguso huu ulifanyika Vienne Ufaransa baada ya mashindano
 • Mtaguso wa Efeso 431 unahesabiwa na Wakristo walio wengi kama mtaguso mkuu wa tatu. Ulifanyika Efeso katika mkoa wa Asia Ndogo, kwa amri ya kaisari
 • Mtaguso wa Trento uliofanyika kwa kwikwi kuanzia mwaka 1545 hadi 1563 unahesabiwa na Kanisa Katoliki kuwa mtaguso mkuu wa kumi na tisa. Miaka hiyo maaskofu
 • mengine. 1. Mtaguso wa kwanza wa Nikea mwaka 325 2. Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli 381 3. Mtaguso wa Efeso 431 4. Mtaguso wa Kalsedonia 451 5
 • Mtaguso wa kwanza wa Laterano unahesabiwa na Kanisa Katoliki mtaguso mkuu wa tisa katika historia yake, wa kwanza kufanyika Magharibi. Ulianza tarehe 18
 • Mtaguso wa Yerusalemu au Mtaguso wa mitume ni jina linalotumika kwa mkutano uliofanyika mwaka 49 au 50 ili kuondoa tofauti za misimamo kati ya Wakristo
 • Mtaguso wa nne wa Konstantinopoli ni jina linalotumiwa na Wakristo kwa namna tofauti, kadiri wanavyokubali au kukataa uhalali na uekumeni wa mitaguso fulanifulani

Users also searched:

...

FAHAMU MAANA YA MTAGUSO Radio Maria Tanzania.

Mtaguso ni mkutano wa viongozi wa Kanisa hasa Baba Mtakatifu, Makardinali, ma Askofu pamoja na Wakristo Mtaguso wa Kalsedonia 451.


...