Back

ⓘ Mtaguso wa pili wa Konstantinopoli uliitishwa na kaisari Justiniani I mwaka 553 kwa lengo la kupatanisha tena na Kanisa Katoliki Wakristo wote wa Misri, Syria n ..
Mtaguso wa pili wa Konstantinopoli
                                     

ⓘ Mtaguso wa pili wa Konstantinopoli

Mtaguso wa pili wa Konstantinopoli uliitishwa na kaisari Justiniani I mwaka 553 kwa lengo la kupatanisha tena na Kanisa Katoliki Wakristo wote wa Misri, Syria n.k. waliojitenga miaka 100 iliyopita kufuatana na Mtaguso wa Kalsedonia.

Kwa ajili hiyo kaisari huyo alifanya yalaaniwe maandishi ya Wanestori watatu Teodoro wa Mopsuestia, Teodoreto wa Kiro na Iba wa Edesa yaliyochukiwa sana na Wamisri.

Pia mtaguso mkuu huo ulilaani baadhi ya mafundisho wa Origene.

Walihudhuria maaskofu 168; kati yao 11 walitokea magharibi. Kumbe Papa Vigili 537-555, pamoja na maaskofu wengine 12 wa magharibi walikataa kuhudhuria ingawa walikuwepo Konstantinopoli, ila mwaka uliofuata alikubali maamuzi ya mtaguso.

Hatimaye Papa Gregori I 590-604 aliutambua kama mtaguso mkuu kwa sababu haukuharibu kitu. Hivyo Wakristo wengi wanahesabu mtaguso huo kuwa wa tano kati ya Mitaguso ya kiekumeni, ingawa lengo halikufikiwa, kwa kuwa Wamisri waliendelea kukataa mtaguso wa Kalsedonia.

                                     
 • wa imani Mtu wa hamaki na mwenye uwezo wa kufanikisha mambo yoyote, ni maarufu hasa kwa kumkomesha Nestori wa Konstantinopoli katika Mtaguso wa Efeso
 • tarehe ya kifo chake. Alisimamia Mtaguso wa pili wa Konstantinopoli 381 ulioitishwa na kaisari Theodosius I.. Watakatifu wa Agano la Kale Orodha ya Watakatifu
 • 241. 553 - Mwanzo wa Mtaguso wa pili wa Konstantinopoli 1925 - Ruth First, mwandishi wa Afrika Kusini 1929 - Ronald Golias, mwigizaji wa filamu kutoka Brazil
 • ufanyike mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli 383 ambao ni wa pili kati ya mitaguso ya kiekumene, nao ukasisitiza na kukamilisha imani ya mtaguso wa kwanza
 • la Antiokia Mwaka huo Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli ulifanya mji huo kuwa na Patriarki wake, wa pili baada ya askofu wa Roma tu. Hapo liturujia
 • kardinali wa kwanza kati ya wale aliowateua tarehe 15 Desemba 1958. Chini ya Papa huyo, kardinali Montini alihusika sana na maandalizi ya Mtaguso wa pili wa Vatikano
 • asiweze kuendelea kuitetea wala kwa maandishi wala kwa sauti. Mtaguso wa tatu wa Konstantinopoli ulimpa ushindi baada ya kifo chake. Tangu kale anaheshimiwa
 • haraka haikusaidia kuzifanikisha, kwa mfano katika Mtaguso wa pili wa Lyon 1274 na katika Mtaguso wa Firenze 1431 - 1449 Njia ya taratibu iliyoshikwa
 • wa taa iliyohesabiwa kati ya maajabu saba ya dunia ya kale. Aleksandria ikawa jimbo kuu la pili kwa umuhimu katika Kanisa baada ya Roma hadi mtaguso wa
 • kulenga umoja na madhehebu mengine, bali linafuata njia za ekumeni. Mtaguso wa pili wa Vatikano uliyazungumzia Makanisa Katoliki ya Mashariki na kuyatolea
 • katika ushirika kamili na Papa wa Roma. Ushirika huo ulidhoofika baada ya Mtaguso wa Kalsedonia 451 hasa kutokana na ugumu wa mawasiliano. Lakini haukuisha

Users also searched:

...

FAHAMU MAANA YA MTAGUSO Radio Maria Tanzania.

Mtaguso wa tatu wa Konstantinopoli 680 681 7. Mtaguso wa pili wa Nikea 787 ​. Makanisa ya Waorthodoksi wa mashariki hukubali mitaguso. Papa Francis afanya marekebisho ya Sheria za Kanisa Katoliki. Kanisa Katoliki likiwa la zamani Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki Konstantinopoli, Aleksandria, Antiokia na Yerusalemu ulisababisha mafarakano Mbele ya changamoto hizo, Mtaguso wa pili wa Vatikano.


...