Back

ⓘ Mtaguso wa pili wa Nisea uliitishwa na malkia Irene wa Bizanti mwaka 787, ili kujadili matumizi ya picha takatifu na sanamu katika Ukristo, kutokana na ombi la ..
Mtaguso wa pili wa Nisea
                                     

ⓘ Mtaguso wa pili wa Nisea

Mtaguso wa pili wa Nisea uliitishwa na malkia Irene wa Bizanti mwaka 787, ili kujadili matumizi ya picha takatifu na sanamu katika Ukristo, kutokana na ombi la Papa Adrian I.

Wakristo wengi wanauhesabu kuwa wa saba kati ya Mitaguso ya kiekumeni. Ni wa mwisho kufanyika wakati wa mababu wa Kanisa.

                                     

1. Historia

Mtaguso mkuu huo ulihitajika ili kumaliza mabishano makali kuhusu sanamu za Kikristo yaliyochukua zaidi ya miaka 100 hasa katika Dola la Roma Mashariki yakimalizika mwaka 843 tu.

Chanzo ni uamuzi wa kaisari Leo III wa Bizanti 717-741 wa kuteketeza sanamu zote ili kujilinganisha na Waislamu waliotishia utawala wake na kujenga uhusiano mzuri nao.

Ndio mwanzo wa mabishano makubwa yasiyoishia katika hoja na maandishi, bali yalichukua uhai wa watu, hasa waliodhulumiwa na serikali.

Patriarki wa Konstantinopoli alilazimika kujiuzulu, lakini uamuzi wa kaisari ulizidi kupingwa na Wakristo wengi, hasa wamonaki na mwanateolojia Yohane wa Damasko. Mapapa wa Roma pia walipinga uamuzi huo.

Sera ya dola ilibadilika aliposhika uongozi Irene kwa niaba ya mtoto wake mdogo Konstantino VI wa Bizanti.

Mtaguso ulianza Konstantinopoli mwaka 786, lakini ulipoingiliwa na jeshi waliowaunga mkono maaskofu wengi waliopinga sanamu, Irene aliuhamishia Nisea ambapo vilifanyika vikao 7 kuanzia tarehe 28 Septemba 787. Cha mwisho kilifanyika katika ikulu tarehe 23 Oktoba 787.

Pamoja na maaskofu 300 hivi wa dola hilo, walihudhuria wamonaki wengi. Papa alituma mabalozi wake wawili na barua moja.

Mtaguso ulitofautisha heshima inayokubalika kwa sanamu na ibada isiyovumilika. Hoja kuu ni kwamba sanamu si kitu, ila inamwakilisha yule aliyechorwa ndani yake. Kimsingi sanamu zinakubalika kutokana na umwilisho wa Mwana wa Mungu uliomfanya atwae sura na kuonekana.

Mtaguso ulichukua pia maamuzi mbalimbali ili kurekebisha Kanisa.

                                     

2. Viungo vya nje

 • Mtaguso wa pili wa Nisea katika Mababu wa Kanisa
 • Mtaguso wa pili wa Nisea katika Catholic Encyclopedia
 • Mtaguso wa pili wa Nisea - 787 B.K.
 • Taarifa zaidi kutoka vyanzo vya Karne za Kati
                                     
 • 241. 553 - Mwanzo wa Mtaguso wa pili wa Konstantinopoli 1925 - Ruth First, mwandishi wa Afrika Kusini 1929 - Ronald Golias, mwigizaji wa filamu kutoka Brazil
 • mtaguso mkuu wa Nisea Baada ya farakano la mwaka 1054 kati ya Kanisa la Kilatini na Makanisa ya Mashariki ambayo yalikuwa bado na ushirika na Papa wa
 • pamoja na mtoto wa ndugu yake, Theodoro wa Studion wakati wa dhuluma ya serikali ya Dola la Roma Mashariki na katika mtaguso wa pili wa Nisea Tangu kale
 • aliitisha mtaguso mkuu wa kwanza uliofanyika mwaka 325 huko Nisea Mtaguso huo ulitunga kanuni ya imani iliyokiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu kwa maana
 • na ya 8 likamalizika katika mtaguso wa pili wa Nisea Hata hivyo, baadaye lilizuka tena na tena, hivi kwamba msimamo wa madhehebu ni tofauti sana. Simba - mtu
 • chombo cha neema kwa kuitiwa Roho Mtakatifu. Alipewa ushindi na Mtaguso wa pili wa Nisea 787 baada ya kifo chake. Wewe, Bwana, ulinitoa katika viuno vya
 • wa mabishano makubwa yasiyoishia katika hoja na maandishi, bali yalichukua uhai wa watu, hasa waliodhulumiwa na serikali. Hatimaye Mtaguso wa pili wa
 • Konstantino aliitisha huko Nisea mtaguso mkuu wa kwanza wa maaskofu wote ili kurudisha umoja wa Kanisa uliovurugwa na uzushi wa Ario kuhusu Yesu Kristo.
 • hiyo fomula rasmi ambayo ilipitishwa na Mtaguso wa kwanza wa Nisea 325 ikakamilishwa na Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli 381 ili kubainisha imani
 • wengi wa dola lake walipinga uamuzi huo, wakiungwa mkono na Papa Gregori III. Hatimaye Mtaguso wa pili wa Nisea 787 ulitetea na kupitisha uhalali wa picha

Users also searched:

...

Mtaguso wa Kwanza wa Nicea wa Mwaka 325 ndio uliamua kwamba Pasaka itasherehekewa Jumapili ya kwanza baada ya mwezi mpevu wa.


...