Back

ⓘ M-pesa ni huduma ya kutuma pesa kwa kutumia simu ya mkononi inayotolewa na kampuni ya mawasiliano ya Safaricom. Kenya ndiyo nchi ya kwanza kuwahi kutumia huduma ..
M-pesa
                                     

ⓘ M-pesa

M-pesa ni huduma ya kutuma pesa kwa kutumia simu ya mkononi inayotolewa na kampuni ya mawasiliano ya Safaricom. Kenya ndiyo nchi ya kwanza kuwahi kutumia huduma hii maarufu ambayo ilizinduliwa mwezi Aprili mwaka wa 2008 kwa ushirikiano kati ya Safaricom na Vodafone. Tangu wakati huo, Mpesa imetia fora sana hasa kwa wananchi wa mapato ya chini wasio na akaunti za benki. Kulingana na takwimu rasmi za Safaricom, Mpesa ina wateja zaidi ya milioni Saba na imewezesha wakenya kutuma na kupokea takriban shilingi bilioni 230 kufikia Agosti 2009. Mwaka huu, Safaricom iliboresha huduma hii zaidi hivi kwamba wakenya wanaweza kupokea pesa moja kwa moja kutoka kwa jamaa zao walioko nchini Uingereza.

Baadhi ya mambo yanayoipa umaarufu huduma hii ni kama vile urahisi wa kuitumia na kwamba mtu hahitaji kuwa na akaunti ya benki kutuma au kupokea pesa. Isitoshe, usalama wake ni wa hali ya juu na anayeitumia hupokea ujumbe mfupi papo hapo kudhibitisha kuwa ametuma au kupokea kiasi fulani cha pesa kwa/kutoka mtu fulani. Kwa sasa, huduma hii imepanuliwa na kuwawezesha wakenya kulipia bidhaa na huduma kadha wa kadha, kama vile stima, maji, posta, bima, nauli, karo, na hata kulipia mikopo ya benki na mishahara kwa wafanyikazi. Mtu anaweza kuweka, kutoa na kutuma pesa kupitia wakala wa M-pesa alie idhinishwa na kuthibitishwa na safaricome au vodacome kwa upande wa Tanzania kwakufuata kanuni na taratibu zilizo wekwa na Makampuni ya mawasiliano hayo.

                                     

1. Safaricom

Kampuni ya Safaricom, ambayo ilisajiliwa mwaka jana katika Soko la Hisa la Nairobi inaongozwa na Bw.Michael Joseph, Afisa Mkuu Mtendaji ambaye amekuwa katika hatamu za uongozi wa kampuni hii yenye mgawo mkubwa zaidi wa wateja nchini Kenya tangu ilipoanzishwa mwaka wa 2000. Kuimarika kwake kumeifanya kutambulika kama Kampuni inayoheshimika zaidi katika Afrika Mashariki kwa miaka mitatu mfululizo.