Back

ⓘ Mtaguso wa kwanza wa Laterano unahesabiwa na Kanisa Katoliki mtaguso mkuu wa tisa katika historia yake, wa kwanza kufanyika Magharibi. Ulianza tarehe 18 Machi u ..
Mtaguso wa kwanza wa Laterano
                                     

ⓘ Mtaguso wa kwanza wa Laterano

Mtaguso wa kwanza wa Laterano unahesabiwa na Kanisa Katoliki mtaguso mkuu wa tisa katika historia yake, wa kwanza kufanyika Magharibi. Ulianza tarehe 18 Machi ukamalizika tarehe 11 Aprili 1123.

Mahali pake ni kwenye Kanisa kuu la Roma huko Laterano, mtaa wa Roma Italia alipokuwa anaishi askofu wake. Hukohuko baadaye ilifanyika mitaguso mingine minne ya Karne za Kati. Umuhimu wa kanisa hilo ulipungua hasa baada ya Papa kuhamia Vatikano.

                                     

1. Historia

Mtaguso uliitishwa na Papa Callixtus II 1119-1124 mnamo Desemba 1122, mara baada ya Mapatano ya Worms, ya kwanza kufanyika kati ya Papa na Dola Takatifu la Kirumi, iliyofurahisha sana wanakanisa, hata mwaka huo ulitajwa kuwa mwanzo wa kipindi kipya.

Mapatano hayo yalikomesha desturi ya walei kuteua viongozi wa Kanisa na wa utawa, yakitenganisha shughuli za kiserikali na zile za kidini, na kukubali kwamba mamlaka ya kiroho inatokana na daraja takatifu.

Ili kuthibitisha mapatano hayo, Papa alialika Roma maaskofu wote wa Magharibi. Waliohudhuria kweli walikuwa zaidi ya 900, wakiwemo maaskofu zaidi ya 300 na maabati 600 hivi. Papa mwenyewe aliendesha vikao.

Hakuna hati za mtaguso, ila matunda yake. Tunachojua ni kwamba Mapatano hayo yalisomwa yakapitishwa rasmi, pamoja na kanuni 22 au 25, ambazo nyingi zilikuwa zimeshapitishwa zamani.

                                     
 • Mtaguso wa Trento uliofanyika kwa kwikwi kuanzia mwaka 1545 hadi 1563 unahesabiwa na Kanisa Katoliki kuwa mtaguso mkuu wa kumi na tisa. Miaka hiyo maaskofu
 • agizo la Mtaguso IV wa Laterano ndugu hao walipaswa kujichagulia kanuni iliyowahi kukubaliwa na Kanisa, wakaamua kushika ile ya Agostino wa Hippo, wakiiongezea
 • agizo la Mtaguso IV wa Laterano ndugu hao walipaswa kujichagulia kanuni iliyowahi kukubaliwa na Kanisa, wakaamua kushika ile ya Agostino wa Hippo, wakiiongezea
 • 1215 Novemba ulifanyika Mtaguso Mkuu wa IV wa Laterano ambao Fransisko alihudhuria pamoja na maaskofu na wakuu wengine wa mashirika labda ndipo alipofunga
 • walikwenda Roma, walipokaribishwa na Papa Alexander III. Mwaka huohuo mtaguso wa tatu wa Laterano ulikataa baadhi ya mawazo ya Valdo, bila kulaani tapo lenyewe
 • walikwenda Roma, walipokaribishwa na Papa Alexander III. Mwaka huohuo mtaguso wa tatu wa Laterano ulikataa baadhi ya mawazo ya Valdo, bila kulaani tapo lenyewe
 • uombaji wa msaada kwa ajili ya maskini, ghala za kugawia chakula bure, mafunzo kwa watoto fukara na kwa wanaosomea upadri n.k. Mtaguso wa tano wa Laterano ulitofautisha
 • upande wa elimu, utume na uongozi. Jambo muhimu zaidi, lilimzaa mtakatifu wa kwanza bradha Felix wa Cantalice 1587 kielelezo cha unyofu. Mtaguso wa Trento
 • ubavu wa mtakatifu huyo. Halafu wakaendelea kupigania ufukara mkuu dhidi ya mashauri ya watu mbalimbali. Ni kwamba baada ya Mtaguso IV wa Laterano 1215
 • sala na sadaka, wakichangia urekebisho wa Kanisa bila ya kutoka nje ya kiota chao. Baada ya Mtaguso IV wa Laterano 1215 kukataza kanuni mpya iliwabidi
 • mwanahistoria wa kwanza kuorodhesha Mapapa bila kuacha pengo. Orodha yake ilikwenda hadi mwaka wa 1049 ikimtaja Papa Leo IX kama Papa wa 154. Kulingana

Users also searched:

...

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate Like.

Karibuni ulikuwa Mtaguso wa pili wa Vatikano uliofanyika Roma kati ya 1962 na 1965 na kuleta hali Mtaguso wa kwanza wa Laterano 1123. FAHAMU MAANA YA MTAGUSO Radio Maria Tanzania. Kwanza ni huo mtaguso wa awali ambao nimesema baadhi ya wataalamu wa mambo ya Mtaguso mkuu wa Laterano V 1512 1517 20.


...