Back

ⓘ Mtaguso wa pili wa Laterano, uliofanyika kuanzia tarehe 4 hadi 11 Aprili 1139 chini ya Papa Inosenti II, unahesabiwa na Kanisa Katoliki kuwa mtaguso mkuu wa kum ..
Mtaguso wa pili wa Laterano
                                     

ⓘ Mtaguso wa pili wa Laterano

Mtaguso wa pili wa Laterano, uliofanyika kuanzia tarehe 4 hadi 11 Aprili 1139 chini ya Papa Inosenti II, unahesabiwa na Kanisa Katoliki kuwa mtaguso mkuu wa kumi.

Ni wa pili kufanyika Magharibi, kwenye Kanisa kuu la Roma Italia.

                                     

1. Historia

Mtaguso ulihitajika kutokana na farakano lililotokea mwaka 1130 alipofariki Papa Honori II 1124-1130: hapo makardinali waligawanyika kuhusu Mapatano ya Worms, ambayo mwaka 1122 yalikuwa yamekomesha Mashindano kuhusu uteuzi wa maaskofu.

Isitoshe, kulikuwa na ushindani kati ya koo mbili za Roma, yaani Frangipane na Pierleoni.

Tarehe 14 Februari 1130, makardinali 16 waliosimama upande wa familia ya Frangipane walimchagua Gregorio Papareschi, aliyejiita Papa Inosenti II.

Saa chache baadaye, Pietro Pierleoni alichaguliwa na makardinali wengine na kujiita papa Anakleti II.

Hatimaye, kwa msaada wa Bernardo wa Clairvaux, Inosenti II alishinda na kukubaliwa na wengi, ingawa hakuweza kuhamia Roma mpaka baada ya mpinzani wake kufa 1138.

Mtaguso ulipaswa kurekebisha matokeo ya farakano hilo. Basi Inosenti II alifungua kikao na kuondoa madarakani maaskofu waliomfuata mpinzani wake.

Halafu papa alikusudia kuendeleza juhudi za urekebisho za Mtaguso wa kwanza wa Laterano. Hivyo zikapitishwa kanuni 30, ambazo nyingi kati yake zilikuwa za kurudia zile za zamani kuhusu usimoni, mapadri wenye wake n.k.

                                     
  • Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli ndio wa pili katika orodha ya mitaguso ya kiekumene ya Kanisa wakati wa mababu wake. Uliitishwa na kaisari Theodosius
  • Mtaguso wa Kalsedonia unahesabiwa na Wakristo wengi kuwa wa nne kati ya mitaguso ya kiekumene katika historia ya Kanisa. Ulifanyika Kalsedonia leo katika
  • 1215 Novemba ulifanyika Mtaguso Mkuu wa IV wa Laterano ambao Fransisko alihudhuria pamoja na maaskofu na wakuu wengine wa mashirika labda ndipo alipofunga
  • uombaji wa msaada kwa ajili ya maskini, ghala za kugawia chakula bure, mafunzo kwa watoto fukara na kwa wanaosomea upadri n.k. Mtaguso wa tano wa Laterano ulitofautisha
  • watu wa kuhamahama, na kwa wahamiaji wa nchi zilizoendelea, huduma hospitalini n.k. Baada ya vita vikuu vya pili na hasa mara baada ya Mtaguso karama
  • sala na sadaka, wakichangia urekebisho wa Kanisa bila ya kutoka nje ya kiota chao. Baada ya Mtaguso IV wa Laterano 1215 kukataza kanuni mpya iliwabidi
  • mwanahistoria wa kwanza kuorodhesha Mapapa bila kuacha pengo. Orodha yake ilikwenda hadi mwaka wa 1049 ikimtaja Papa Leo IX kama Papa wa 154. Kulingana

Users also searched:

...

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate Like.

Mtaguso ni mkutano wa viongozi wa Kanisa hasa Baba Mtakatifu, Makardinali, ma Askofu karibuni ulikuwa Mtaguso wa pili wa Vatikano uliofanyika Roma kati ya 1962 na 1965 na Mtaguso wa kwanza wa Laterano 1123. FAHAMU MAANA YA MTAGUSO Radio Maria Tanzania. Kwanza ni huo mtaguso wa awali ambao nimesema baadhi ya wataalamu wa mambo ya Mtaguso mkuu wa Laterano V 1512 1517 20.


...