Back

ⓘ Mtaguso wa nne wa Laterano unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na mbili. Uliitishwa na Papa Inosenti III 1198-1216 kama kilele cha kazi yak ..
Mtaguso wa nne wa Laterano
                                     

ⓘ Mtaguso wa nne wa Laterano

Mtaguso wa nne wa Laterano unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na mbili.

Uliitishwa na Papa Inosenti III 1198-1216 kama kilele cha kazi yake.

Ulihudhuriwa na maaskofu zaidi ya 400 wakiwemo mapatriarki wa Kilatini wa Konstantinopoli na Yerusalemu na wawakilishi wa wale wa Antiokia na Aleksandria, na wakuu wa watawa zaidi ya 800, mbali na mabalozi wa watawala wa nchi mbalimbali.

Mada kuu zilikuwa Vita vya msalaba, Mashindano kuhusu uteuzi wa viongozi wa Kanisa, mamlaka ya Papa, mwenendo wa makleri, mashirika ya kitawa, imani kuhusu ekaristi n.k., na wajibu wa Wakristo wote kupokea sakramenti ya kitubio walau mara moja kwa mwaka.

Kutokana na wingi na umuhimu wa mafundisho na maamuzi yaliyotolewa, mtaguso huo unahesabiwa kuwa kati ya ile iliyoathiri zaidi Kanisa hadi leo.

                                     

1. Historia

Mtaguso uliitishwa mjini Roma na Papa Inosenti III kwa hati Vineam Domini Sabaoth, iliyotolewa tarehe 19 Aprili 1213.

Papa mwenyewe ndiye aliyefungua kikao kwa hotuba ya kusisimua tarehe 11 Novemba 1215, naye tarehe 30 Novemba alipendekeza kanuni 70 ambazo zilipitishwa bila ya kupingwa.

Hivyo mtaguso huo ulizidi kukusanya mamlaka ya Kanisa mikononi mwa Papa.

                                     

2. Viungo vya nje

  • Enchiridion symbolorum, definitionum et declarationum de rebus fidei et morum 800-815 Mafundisho muhimu ya mtaguso huo kwa Kilatini
  • Mtaguso wa nne wa Laterano katika Catholic Encyclopedia.
                                     
  • Mtaguso wa nne wa Konstantinopoli ni jina linalotumiwa na Wakristo kwa namna tofauti, kadiri wanavyokubali au kukataa uhalali na uekumeni wa mitaguso fulanifulani
  • 1215 Novemba ulifanyika Mtaguso Mkuu wa IV wa Laterano ambao Fransisko alihudhuria pamoja na maaskofu na wakuu wengine wa mashirika labda ndipo alipofunga
  • uombaji wa msaada kwa ajili ya maskini, ghala za kugawia chakula bure, mafunzo kwa watoto fukara na kwa wanaosomea upadri n.k. Mtaguso wa tano wa Laterano ulitofautisha
  • ubavu wa mtakatifu huyo. Halafu wakaendelea kupigania ufukara mkuu dhidi ya mashauri ya watu mbalimbali. Ni kwamba baada ya Mtaguso IV wa Laterano 1215
  • 1274 Vienne 1311 - 1312 Konstans 1414 - 1418 Firenze 1431 - 1445 na Laterano V 1512 - 1517 Vilevile ndugu wengine walitetea haki za Papa dhidi ya upinzani
  • sala na sadaka, wakichangia urekebisho wa Kanisa bila ya kutoka nje ya kiota chao. Baada ya Mtaguso IV wa Laterano 1215 kukataza kanuni mpya iliwabidi
  • mwanahistoria wa kwanza kuorodhesha Mapapa bila kuacha pengo. Orodha yake ilikwenda hadi mwaka wa 1049 ikimtaja Papa Leo IX kama Papa wa 154. Kulingana

Users also searched:

...

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate Like.

Na nne ni Mitaguso mikuu, mitaguso ya kipindi cha ukomavu wa kanisa. Orodha ya Mtaguso mkuu wa Laterano V 1512 1517 20. FAHAMU MAANA YA MTAGUSO Radio Maria Tanzania. Возможно, вы имели в виду:. Mtaguso ni mkutano wa viongozi wa Kanisa hasa Baba Mtakatifu, Makardinali, ma Askofu pamoja na Mtaguso wa nne wa Laterano 1215.


...