Back

ⓘ Mtaguso wa tano wa Laterano ulifanyika kuanzia mwaka 1512 hadi 1517 huko Roma, kwenye Basilika la Mt. Yohane huko Laterano ambalo ndilo kanisa kuu la Jimbo Kato ..
Mtaguso wa tano wa Laterano
                                     

ⓘ Mtaguso wa tano wa Laterano

Mtaguso wa tano wa Laterano ulifanyika kuanzia mwaka 1512 hadi 1517 huko Roma, kwenye Basilika la Mt. Yohane huko Laterano ambalo ndilo kanisa kuu la Jimbo Katoliki la Roma.

Kanisa Katoliki linauhesabu kama mtaguso mkuu wa kumi na nane.

Uliitishwa na Papa Julius II 1503-1513 ambaye alianza kuusimamia tarehe 3 Mei 1512. Baada ya kifo chake, uliendelezwa na Papa Leo X 1513-1521 hadi kikao cha 12 na cha mwisho kilichofanyika tarehe 16 Machi 1517.

Ulihudhuriwa na maaskofu 100 hivi, wengi wao wakitokea Italia. Kutofika kwa wajumbe kutoka nchi nyingine, pamoja na wengi kukosa nia ya kujirekebisha, kulichangia kufanya utekelezaji wa maamuzi ya mtaguso ushindikane.

Maamuzi hayo yalitolewa kwa hati za Papa. Mengine yanahusu mafundisho ya imani, mengine maagizo ya urekebisho wa Kanisa.

                                     

1. "Kitaguso" cha Pisa

Kwa kuwa Papa Julius II alikuwa hatekelezi kiapo chake cha kuitisha mtaguso kwa ajili ya urekebisho, baadhi ya makardinali, wakihimizwa na watawala wa Ujerumani na Ufaransa, waliuitisha huko Pisa Italia kuanzia tarehe 1 Septemba 1511. Walikusanyika wachache tarehe 1 Oktoba, halafu katika kikao cha nane walimsimamisha Papa wakahamia Lyon Ufaransa.

                                     

2. Kuitisha mtaguso

Papa aliitikia" kitaguso” hicho kwa hati ya tarehe 18 Julai 1511, ambayo pamoja na kukipinga na kujitetea aliitisha mtaguso mkuu ukusanyike tarehe 19 Aprili 1512 huko Laterano.

                                     

3. Mtaguso wenyewe

Vita vilichelewesha mwanzo wa mtaguso hadi tarehe 3 Mei 1512, walipokusanyika katika basilika la Laterano makardinali 15, mapatriarki 2, maaskofu wakuu 10, maaskofu 56, maabati na wakuu wa mashirika ya kitawa wachache pamoja na mabalozi wa nchi 3. Mwisho walikuwepo makardinali 23 na maaskofu 122.

                                     

4. Matokeo

Utekelezaji wa maagizo ya mtaguso ulikuwa mdogo sana, la sivyo pengine Matengenezo ya Kiprotestanti yasingetokea. Ukweli ni kwamba Martin Luther aliyaanzisha miezi sita tu baada ya mtaguso kwisha.

                                     
  • 590 - 604 aliutambua kama mtaguso mkuu kwa sababu haukuharibu kitu. Hivyo Wakristo wengi wanahesabu mtaguso huo kuwa wa tano kati ya Mitaguso ya kiekumeni
  • 1215 Novemba ulifanyika Mtaguso Mkuu wa IV wa Laterano ambao Fransisko alihudhuria pamoja na maaskofu na wakuu wengine wa mashirika labda ndipo alipofunga
  • uombaji wa msaada kwa ajili ya maskini, ghala za kugawia chakula bure, mafunzo kwa watoto fukara na kwa wanaosomea upadri n.k. Mtaguso wa tano wa Laterano ulitofautisha
  • sala na sadaka, wakichangia urekebisho wa Kanisa bila ya kutoka nje ya kiota chao. Baada ya Mtaguso IV wa Laterano 1215 kukataza kanuni mpya iliwabidi
  • mwanahistoria wa kwanza kuorodhesha Mapapa bila kuacha pengo. Orodha yake ilikwenda hadi mwaka wa 1049 ikimtaja Papa Leo IX kama Papa wa 154. Kulingana

Users also searched:

...

FAHAMU MAANA YA MTAGUSO Radio Maria Tanzania.

Mtaguso ni mkutano wa viongozi wa Kanisa hasa Baba Mtakatifu, Mtaguso wa tatu wa Laterano 1179 12. Mtaguso wa tano wa Laterano.


...