Back

ⓘ Nabii Baruku mwana wa Neria alikuwa mwandishi wa karne ya 6 KK, maarufu kama karani, mwanafunzi na rafiki mpendwa wa nabii Yeremia. Tangu kale anaheshimiwa kama ..
Nabii Baruku
                                     

ⓘ Nabii Baruku

Nabii Baruku mwana wa Neria alikuwa mwandishi wa karne ya 6 KK, maarufu kama karani, mwanafunzi na rafiki mpendwa wa nabii Yeremia.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu na madhehebu mbalimbali ya Ukristo.

Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 11 Oktoba.

                                     

1. Maisha

Kadiri ya Yosefu Flavius, alikuwa sharifu wa Uyahudi, mwana wa Neria na ndugu wa Seraia mwana wa Neria, waziri wa mfalme Zedekia wa Ufalme wa Yuda.

Baruku aliandika maneno ya Yeremia alivyoagizwa naye akabaki mwaminifu kwake hata katika dhuluma. Yeremia alipokuwa mafichoni alimtuma kusoma katika Hekalu la Yerusalemu utabiri wa adhabu dhidi ya mfalme Yehoyakimu Huenda kama shukrani kwa kutekeleza agizo hilo gumu, Yeremia alimtabiria mema.

Wote wawili walishuhudia maangamizi ya Yerusalemu 587 KK wakabaki pamoja baada yakempaka walipopelekwa nchini Misri.

Uhusiano huo ulifanya Baruku aheshimiwe sana na vizazi vilivyofuata, hata vitabu viliandikwa kwa jina lake:

  • 4 Baruku, au Paraleipomena of Jeremiah
  • Kitabu cha Baruku au 1 Baruku, ambacho ni kati ya deuterokanoni, vinavyoheshimiwa na Kanisa Katoliki na wengineo kama sehemu ya Biblia ya Kikristo
  • 3 Baruku, au Greek Apocalypse of Baruch
  • 2 Baruku, au Syriac Apocalypse of Baruch
                                     

2. Marejeo

  • Baruku katika Catholic Encyclopedia.
  • Shanks, Hershel. Fingerprint of Jeremiah’s Scribe. Biblical Archeology Review 2 1996: 36-38.
  • Shanks, Hershel, Jeremiahs Scribe and Confidant Speaks from a Hoard of Clay Bullae, Biblical Archaeology Review 13.5 1987 58-65.
  • Avigad, Nahman, Jerahmeel & Baruch, Biblical Archaeology Review 42.2 1979. 114-118.
  • Wright, J. Edward, Baruch ben Neriah: From Biblical Scribe to Apocalyptic Seer University of South Carolina Press, 2003 ISBN 1-57003-479-6
  • The Seal of Seraiah, Eretz Israel 14 1978, Ginsberg festschrift 86-87.