Back

ⓘ Farakano la mwaka 1054 lilitokea hasa kati ya Papa Leo IX wa Roma na Patriarki Mikaeli Serulari wa Konstantinopoli likasababisha ushirika kati ya Ukristo wa Mag ..
Farakano la mwaka 1054
                                     

ⓘ Farakano la mwaka 1054

Farakano la mwaka 1054 lilitokea hasa kati ya Papa Leo IX wa Roma na Patriarki Mikaeli Serulari wa Konstantinopoli likasababisha ushirika kati ya Ukristo wa Magharibi na sehemu kubwa ya Ukristo wa Mashariki usiendelee kuwa kamili hadi leo.

Mahusiano yalikuwa yamezidi kuharibika tangu karne ya 4 ambapo ulianza ushindani kati ya miji hiyo miwili iliyokuwa kwa pamoja makao makuu ya Dola la Roma.

Maelekeo tofauti katika teolojia, maisha ya kiroho n.k. yalitumika kama visingizio katika kulaumiana, na hata kufarakana kwa muda.

Hatimaye mabalozi waliotumwa na Papa, ingawa hawakuwa na mamlaka hiyo, waliacha juu ya altare ya kanisa kuu la Konstantinopoli hati ya kumtenga Patriarki na Kanisa Katoliki, naye akaitikia kwa kumtenga Papa na Kanisa la Orthodoksi.

Juhudi mbalimbali za kurudisha umoja zilifanyika katika nafasi mbalimbali, lakini pengine haraka haikusaidia kuzifanikisha, kwa mfano katika Mtaguso wa pili wa Lyon 1274 na katika Mtaguso wa Firenze 1431-1449.

Njia ya taratibu iliyoshikwa pamoja katika karne ya 20 inatia tumaini zaidi. Inakumbukwa hasa tamko la upendo la tarehe 7 Desemba 1965 ambalo Papa Paulo VI na Patriarki Atenagora I kwa pamoja walifuta kutoka kumbukumbu ya Kanisa hati za mwaka 1054 ambazo pande hizo mbili zilitengana.

                                     

1. Marejeo

 • Joseph P. Farrell. God, History, & Dialectic: The Theological Foundations of the Two Europes and Their Cultural Consequences. Bound edition 1997. Electronic edition 2008.
 • Runciman, Steven 1955, The Eastern Schism: A Study of the Papacy and the Eastern Churches during the XIth and XIIth Centuries.
 • Henry Chadwick. East and West: The Making of a Rift in the Church: From Apostolic Times until the Council of Florence. Oxford University Press, 2003.
 • Aidan Nichols. Rome and the Eastern Churches: a Study in Schism. 2010
 • Chrysostom Frank. Orthodox-Catholic Relations: An Orthodox Reflection. 1998
 • John Romanides, The Cure of the Neurobiological Sickness of Religion, the Hellenic Civilization of the Roman Empire, Charlemagnes Lie of 794 and His Lie Today
 • Taft, Robert F 2010, Perceptions and Realities in Orthodox-Catholic Relations Today PDF, Fordham.
                                     

2. Viungo vya nje

 • East–West Schism, Orthodox Church in the Philippines, archived from the original on 2012-09-05, retrieved 2014-07-26.
 • Catholic Encyclopedia: The Eastern Schism
 • The Great Schism, Orthodox SCOBA.
 • Encyclopaedia Britannica: Schism of 1054
 • Joint Catholic-Orthodox Declaration of Pope Paul VI and Ecumenical Patriarch Athenagoras I, 7 December 1965
 • Ware, Bp. Kallistos, Byzantium: The Great Schism, Father Alexander.
 • BBC Radio 4 round table: In Our Time: Schism 16 October 2003 audio
                                     
 • Ucheki. Kanisa hili lilikuwa hapa na vyanzo vyake. Lilitokea baada ya farakano ndani ya Kanisa Katoliki katika Bohemia na Moravia. Nchi hizo mbili zilikuwa
 • Kanisa la Magharibi au Ukristo wa Magharibi linajumlisha Kanisa la Kiroma - Katoliki pamoja na madhehebu ya Kiprotestanti. Huitwa la magharibi kwa sababu
 • miaka 69 1309 - 1378 halafu kwa miaka 38 1378 - 1409 kukawa na Farakano la Kanisa la Magharibi, waamini wengine wakimfuata Papa wa Roma na wengine Antipapa
 • Estonia, Latvia, Namibia na jimbo la North Dakota la Marekani. Muundo wao wa kanisa ni ama dayosisi jimbo au kanisa la kitaifa. Asilimia kubwa ya Walutheri
 • yaliyotengana nalo. Ni kwamba, baada ya utengano wa Mashariki - Magharibi mwaka 1054 muungano mfupi ulikubaliwa kati ya Papa na baadhi ya Maaskofu wa Kiorthodoksi
 • mwaka 1054 wajumbe wa Askofu wa Roma walimtembelea Askofu Mkuu wa Bizanti. Walianza kupingana vikali na mwishoni wakalaaniana. Tangu mwaka ule farakano lilikuwa
 • ni jina linalotumika kwa maana mbalimbali, lakini hasa kumaanisha Kanisa la Kikristo linalokubali mamlaka ya kiroho ya Papa wa Roma kama mkuu wa urika
 • kilichosababisha zaidi farakano si masuala ya imani yaliyojadiliwa na Waprotestanti, bali lawama zao dhidi ya hali mbaya ya Kanisa la wakati huo iliyokuwa
 • kati ya Waprotestanti, hasa lilipofanyika Kongamano la Kimisionari la Kimataifa huko Edimburg, mwaka 1910, ambapo waliohudhuria walisisitiza uhusiano kati
 • hivi duniani kote. Yale makubwa zaidi ni Kanisa la Kiorthodoksi la Kirusi na Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia. 2006 in Angold, Michael: The Cambridge

Users also searched:

...

FAHAMU MAANA YA MTAGUSO Radio Maria Tanzania.

Kanisa Katoliki likiwa la zamani Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki dhidi ya Ukristo ambayo ilianzishwa na Kaisari Nero mwaka 64 na 451, 1054​ yaliyoacha Kanisa Katoliki katika Ulaya magharibi karibu peke yake. halafu kwa miaka 38 1378 1409 kukawa na Farakano la Kanisa la. Papa Francis afanya marekebisho ya Sheria za Kanisa Katoliki. Farakano la mwaka 1054 kati ya Kanisa la Mashariki na Kanisa la Magharibi, pamoja na kulenga umoja uliovunjika na kufundisha dogma mpya.


...