Back

ⓘ Mfumo wa Msimbo wa Posta Tanzania. Mfumo wa Misimbo ya Posta ya Tanzania umeanzishwa tangu mwaka 2012. Msimbo wa posta ni namba iliyochaguliwa kwa kila kata nch ..
Mfumo wa Msimbo wa Posta Tanzania
                                     

ⓘ Mfumo wa Msimbo wa Posta Tanzania

Mfumo wa Misimbo ya Posta ya Tanzania umeanzishwa tangu mwaka 2012. Msimbo wa posta ni namba iliyochaguliwa kwa kila kata nchini. Kila kata ina msimbo wa tarakimu tano.

Nia ni kuwa kila barua inayotumwa nchini Tanzania ionyeshe namba hiyo juu ya bahasha yake kama sehemu ya anwani ya barua au kifurushi ili kurahisisha na kuharakisha usafirishaji.

Namba ya msimbo wa posta ni tofauti na namba ya sanduku la posta; msimbo wa posta unahusu mahali au eneo, ilhali sanduku la posta linamhusu mpokeaji wa barua.

                                     

1. Muundo wa tarakimu katika msimbo wa posta wa Tanzania

Msimbo wa posta nchini Tanzania huwa na tarakimu tano zilizopangwa kufuatana na ngazi za utawala wa nchi:

 • tarakimu za nne na tano pamoja na zinazotangulia zinaonyesha kata.
 • tarakimu ya tatu pamoja na zinazotangulia inaonyesha wilaya au halmashauri
 • Badala ya kata tarakimu kamili zinaweza kuteuliwa pia kwa ajili ya mteja mkubwa anayepokea barua nyingi sana, au eneo maarufu au shughuli maalumu. Mfano ni kampuni kubwa au wizara kuwa na msimbo wa pekee.
 • tarakimu ya kwanza inaonyesha kanda
 • tarakimu ya pili pamoja na inayotangulia inaonyesha mkoa
 • Hakuna misimbo ya pekee kwa kata zote za Tanzania; wakati mwingine kata kadhaa za wilaya ileile zimeunganishwa kwa kazi ya posta na kuwa na msimbo mmoja

Mfano:

6 5 4 0 1 ni msimbo wa posta kwa Kilwa Masoko. 6 ni tarakimu kwa Kanda ya Pwani 6 5 inaonyesha Mkoa wa Lindi 6 5 4 inataja Wilaya ya Kilwa Tarakimu za mwisho 0 1 ni za kata ya Kilwa Masoko.

Ilhali wilaya ya Kilwa huwa na kata 21, misimbo ya kata za Kilwa inaendelea kuanzia 6 5 4 0 1 Kilwa Masoko hadi 6 5 4 2 1 Kibata.

Maana yake kama barua inaonyesha anwani ya "65421 Kibata" inaweza kusafirishwa, si lazima mfanyakazi aulize Kibata iko wapi? Inatosha akijua ni barua kwenda pwani "6" na Mkoa wa Lindi "65". Pale Lindi wanajua wilaya zao na 654 ni Kilwa, vivyo hivyo hao wanajua kata katika eneo lao.

Utaratibu huo unatunza nafasi kwa kuanzishwa kwa vitengo vipya; kanda linaweza kuongezwa mikoa hadi 10, kila mkoa wilaya hadi 10, na kata hadi 100 kila wilaya. Kuna pia nafasi kwa kanda mpya 2.

                                     

2. Kanda

Kanda ni hizi zifuatazo, na kila mkoa wa Tanzania ni sehemu ya kanda fulani:

 • Nyanda za Juu Kusini
 • Zanzibar
 • Ziwa
 • Pwani
 • Kaskazini
 • Dar es Salaam
 • Kati
                                     

3. Viungo vya Nje

 • Kuhusu mfumo wa msimbo wa posta tanzania
 • Tanzania Post Code List chaguo la mikoa
 • Habari za kuanzishwa kwa misimbo ya posta kwenye blogu ya State Africa
                                     
 • Kenya na Tanzania kuna mfumo wa msimbo wa posta mwenye tarakimu tano. Tazama pia Mfumo wa Msimbo wa Posta Tanzania na Mfumo wa Msimbo wa Posta Kenya Kwa
 • Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 18, 976 walioishi humo. Msimbo wa posta ni 25222
 • wikipedia.org wiki Mfumo wa Msimbo wa Posta Tanzania 2002 Population and Housing Census General Report en Government of Tanzania Jalada kutoka ya awali
 • Tanzania imegawanyika katika mikoa 31. Mikoa hiyo yote imegawanyika tena kwenye wilaya 169. Wilaya zimeganyika katika kata kibao. Wakati wa ukoloni wa
 • katika Mkoa wa Tanga, Tanzania Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ina wakazi wapatao 6, 314 waishio humo. Msimbo wa posta ni 21622 Magamba
 • katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania Wakati wa wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 9049 walioishi humo. Msimbo wa posta ni 53213

Users also searched:

jinsi ya kufungua sanduku la posta, posta dar es salaam, shirika la posta tanzania,

...

Online Document Parliament of Tanzania.

Kituo cha Afya Mkamba Wilayani Mkuranga kimefikia hatua ya mwisho za ujenzi wa miundombinu ambapo ujenzi huo umeelekezwa kwenye chumba cha. I CHIEF EDITOR VOLUME 6, ISSUE 1, 2020 RUAHA JOURNAL OF. MAHINDI YA TANZANIA NI SALAMA Akiongea na waandishi wa habari alipotembelea mpaka wa Holili. Namna ya kutumia Mfumo wa Kubadili Tahasusi na Vyuo vya kati Anuani ya Posta: P. O. Box 3070, Moshi. KUCHUNGUZA ATHARI YA KUBADILI MSIMBO KATIKA. Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, naomba kutoa shukrani moja kwa moja kwa kutumia mfumo wa benki ya CRDB. Kigezo linganishi ni wastani wa kipato cha faharisi ya hisa Tanzania kwa anaweza kuwekeza kwa kutumia simu ya mkononi kwa kupiga msimbo Sanduku la Posta 14825. USEMEZANO KATIKA RIWAYA YA KISWAHILI UDOM Repository. Kupata Salary Slip kwa Njia ya Mtandao kwa Watumishi wa Umma. Wizara ya fedha Vote kwa mfano 88Z2 Subvote kwa mfano 5007 Account namba link ujisajili. Anuani ya Posta: S.L.P. 5429. Simu ya​. How Do I Single Mkoa wa Dar es Salaam. Kila mchezo wa Betting na droo za MOJASPESHO, INSTAMOJA, namba hizi kwa kuzingatia njia sahihi utaleta matokeo kwenye mfumo wa Mojabet kwa kutoa seti Kwa kutuma baruapepe kwenda support@.tz, Lucky Games Kukawia, hasara, makosa au kukosa kufanya au iliyofanywa na posta au njia.


...