Back

ⓘ Mapatano ya Laterano kati ya Ufalme wa Italia na Ukulu mtakatifu yanaitwa hivyo kwa sababu yalisainiwa katika jumba la Laterano tarehe 11 Februari 1929. Lengo l ..
Mapatano ya Laterano
                                     

ⓘ Mapatano ya Laterano

Mapatano ya Laterano kati ya Ufalme wa Italia na Ukulu mtakatifu yanaitwa hivyo kwa sababu yalisainiwa katika jumba la Laterano tarehe 11 Februari 1929.

Lengo lake lilikuwa kumaliza suala la Roma lililovuruga Italia tangu mwaka 1870, nchi hiyo ilipoteka mji huo uliotawaliwa na Mapapa kwa karne nyingi.

Kwa mapatano hayo, Papa alikubali mji ubaki mikononi mwa Ufalme, isipokuwa mtaa wa Vatikano na majengo mengine machache. Ndivyo ilivyoundwa na kukubalika kimataifa nchi huru ya Mji wa Vatikani iliyomwezesha Papa kuwa huru katika kuongoza Kanisa Katoliki duniani kote.

Mapatano hayo yaliheshimika hata baada ya serikali ya Ufashisti kuanguka, Italia kugeuka Jamhuri na katiba mpya kutungwa. Tena hiyo ilijumlisha mapatano hayo ndani yake.

                                     

1. Marejeo

  • Zuccotti, Susan 2002. Under His Very Windows: The Vatican and the Holocaust in Italy. New Haven: Yale University Press. ISBN 0-300-09310-1.
  • Latourette, Kenneth Scott. Christianity In a Revolutionary Age A History of Christianity in the 19th and 20th Century: Vol 4 The 20th Century In Europe 1961 pp 32–35, 153, 156, 371
  • Pollard, Jonh F. 2014. The Papacy in the Age of Totalitarianism, 1914-1958. Oxford University Press. ISBN 9780199208562.
  • Riccards, Michael 1998. Vicars of Christ: Popes, Power, and Politics in the Modern World. New York: Crossroad. ISBN 0-8245-1694-X.
  • Pollard, John F. 2005. The Vatican and Italian Fascism, 1929-32. A Study in Conflict. Cambridge University Press. ISBN 978-0521023665.
                                     

2. Viungo vya nje

  • Text in the original language of the Lateran Pacts, including the financial convention and the concordat
  • Text of the Lateran Treaty and other laws and decrees related to Vatican City State
                                     
  • Mtaguso wa kwanza wa Laterano unahesabiwa na Kanisa Katoliki mtaguso mkuu wa tisa katika historia yake, wa kwanza kufanyika Magharibi. Ulianza tarehe 18
  • Mtaguso wa pili wa Laterano uliofanyika kuanzia tarehe 4 hadi 11 Aprili 1139 chini ya Papa Inosenti II 1130 - 1143 unahesabiwa na Kanisa Katoliki kuwa

Users also searched:

...