Back

ⓘ Hati ya Thesalonike ilitolewa tarehe 27 Februari 380 BK. Iliagiza raia wote wa Dola la Roma kukiri imani ya maaskofu wa Roma na Aleksandria, ikifanya Ukristo wa ..
                                     

ⓘ Hati ya Thesalonike

Hati ya Thesalonike ilitolewa tarehe 27 Februari 380 BK. Iliagiza raia wote wa Dola la Roma kukiri imani ya maaskofu wa Roma na Aleksandria, ikifanya Ukristo wa Kikatoliki kuwa dini rasmi ya dola hilo.

                                     

1. Yaliyotangulia

Kaisari Konstantino I aliongokea Ukristo mwaka 312.

KUfikia mwaka 325 uzushi wa padri Ario kuhusu Yesu Kristo ulikuwa umeshaenea kiasi cha kuvuruga Kanisa na hata jamii nzima.

Ili kurudisha amani katika dola, Konstantino aliitisha Mtaguso wa kwanza wa Nisea ili uamue imani sahihi ni ipi. Mtaguso mkuu huo ulitoa Kanuni ya imani ya Nisea iliyokanusha Uario kwa kumkiri Kristo kuwa "Mungu kweli" mwenye "hali moja na Baba".

Hata hivyo mabishano hayakuisha, hivyo Konstantino alidhani amekosea kuunga mkono imani ya Nisea akasimama upande wa Waario akivuta wengi upande huo. Hatimaye, alipobatizwa 337, alimchagua askofu wa Kiario Eusebio wa Nikomedia kumbatiza.

Mrithi wake upande wa mashariki, mwanae Constantius II, alikuwa vilevile mtetezi wa Uario akawa anafukuza maaskofu Wakatoliki.

Mwandamizi wake Kaisari Juliani aliasi kabisa Ukristo na kurudia Upagani wa Ugiriki, pamoja na kulinda dini na madhehebu yoyote.

Aliyemfuata, Kaisari Joviano, alitawala miezi 8 tu, akafuatwa na Kaisari Valens, muumini wa Uario.

Mwaka 379, Valens aliporithiwa na Theodosius I, Uario ulikuwa umeenea sana mashariki, lakini si magharibi. Theodosius, aliyezaliwa Hispania, alikuwa na imani kubwa katika mafundisho ya Nisea. Mnamo Agosti, Gratian, mtawala wa magharibi, alianza kudhulumu wazushi.

                                     

2. Umuhimu

Hati ilitolewa kwa athira ya Acholius, na hivyo ya Pope Damasus I aliyemteua. Ilisisitiza imani moja tu kuwa halali katika dola la Roma, ile "katholiki" yaani, isiyo ya sehemu na "orthodoksi" yaani, sahihi.

Tangu hapo, Theodosius alitumia nguvu nyingi kuzima aina zote za Ukristo tofauti na hiyo, hasa Uario.

Hati ilifuatwa mwaka 381 na Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli, uliothibitisha na kuongezea ungamo la Nisea katika Kanuni ya imani ya Nisea-Konstantinopoli.

Mwaka 383, Kaisari alidai madhehebu mengine yote yampatie maungamo yao ya imani, akayachambua na kuyachoma yote isipokuwa ya Wanovasyani. Hivyo madhehebu hayo hawakuruhusiwa tena kukutana, kuweka mapadri wala kueneza mafundisho yao. Theodosius alikataza wazushi wasiishi tena Konstantinopoli, na miaka 392-394 alitaifisha maabadi yao.

                                     

3. Vyanzo

  • Boyd, William Kenneth 1905. The Ecclesiastical Edicts of the Theodosian Code. Columbia University Press.
  • Ehler, Sidney Zdeneck 1967. Church and State Through the Centuries: A Collection of Historic Documents with Commentaries. ISBN 9780819601896.
  • Ferguson, Everett 1999. Encyclopedia of Early Christianity. Taylor & Francis.
  • Williams, Stephen 1994. Theodosius: The Empire at Bay. B.T. Batsford Ltd. ISBN 0-300-06173-0.
                                     
  • Кирилъ Thesalonike 815 Roma, 14 Februari 869 alikuwa mmisionari, mmonaki na mtaalamu wa Kigiriki aliyeweka msingi wa utamaduni wa Kikristo kati ya mataifa
  • mapambano ya siasa. Mahusiano yaliendelea kuwa magumu. Hatimaye Theodosius I, Kaisari wa Mashariki, alipoangamiza 390 watu 7, 000 huko Thesalonike Ugiriki
  • kutokana na mabishano yao kuhusu Kristo. Mtume Paulo alikuwa amekimbia Thesalonike baada ya wiki 3 tu za utume, hivyo aliogopa kwamba huenda dhuluma zikawakatisha
  • iliyokubaliwa katika Dola la Roma dhuluma dhidi ya Wakristo zilikuwa zimekwisha rasmi mwaka 313 kwa Hati ya Milano iliyotolewa na Konstantino Mkuu ili kuruhusu

Users also searched:

...

Vyuo vikuu nchini haviwatendei haki wasabato?? Page 16.

Huna hoja wewe zaidi ya ujuaji. msifanye watu wote ni wajinga. 1 pale Filipi ​Matendo, 3 pale Thesalonike Matendo 17:2.3, Sabato 78 Yesu Kristo,​aliigongomelea msalabani hati yakutushtaki kwa kutokuishika. Возможно, вы имели в виду:.


...