Back

ⓘ Buruji za falaki ni jina la makundinyota yanayoonekana kwenye ekliptiki zaani njia ya Jua angani na kuunda Zodiaki. Katika maarifa ya unajimu au: falaki, tofaut ..
Buruji za falaki
                                     

ⓘ Buruji za falaki

Buruji za falaki ni jina la makundinyota yanayoonekana kwenye ekliptiki zaani njia ya Jua angani na kuunda Zodiaki.

Katika maarifa ya unajimu au: falaki, tofauti na fani ya sayansi inayoitwa astronomia Waswahili wa kale, pamoja na tamaduni nyingi za zamani, waliamini ya kwamba nyota hizi zina tabia fulani na kuwa na athari juu ya maisha ya binadamu wanaozaliwa chini ya nyota fulani.

Hali halisi Jua linapita katika maeneo ya makundinyota 13 lakini tangu zamani za Babeli idadi ilifupishwa kuwa 12 kwa kusudi la kulingana na kalenda ya miezi 12. Kwa kufikia idadi hii kundinyota la Hawaa Ophiuchus liliondolewa katika idadi ya Zodiaki.

                                     

1. Jina

Kwa jumla majina mengi ya nyota yametokana na urithi wa falaki ya Waarabu. Hao walirithi habari hizi pamoja na mpangilio wa nyota kwenye mzingo wa njia ya jua angani kutoka Ugiriki ya Kale. Asili yake iko katika falaki ya Babeli.

"Buruji" yatokana na Kiarabu برج ", burj, tafsiri ya neno la Kigiriki πυργοι pirgoi, yaani mnara au boma.

                                     

2. Buruji za falaki kwenye njia ya jua angani

Buruji za falaki katika utamaduni wa Waswahili ni kama zifuatazo:

 • Mizani ing. Libra
 • Samaki zamani Hutu, lat. Pisces
 • Thauri ing. Taurus
 • Akarabu ing. Scorpio
 • Jauza ing. Gemini
 • Dalu ing. Aquarius
 • Saratani ing. Cancer
 • Nadhifa ing. Virgo
 • Kondoo zamani Hamali, lat. Aries
 • Simba zamani Asadi, lat. Leo
 • Jadi ing. Capricornus
 • Kausi ing. Sagittarius

Katika unajimu wa siku hizi majina mengi ya kimapokeo katika unajimu wa Afrika ya Mashariki yamesahauliwa na badala yake wapiga falaki wanatumia orodha ya majina ambayo mara nyingi ni tafsiri ya majina ya Kiingereza tu, au pia namna ya kutaja alama ya makundinyota kwa neno la Kiswahili. Isipokuwa Mizani na Mashuke bado ni majina asilia. Majina katika unajimu wa kisasa jinsi yalivyo kawaida ni yafuatayo:

 • Mshale Sagittarius: Nov 22- Des 21
 • Ndoo Aquarius:Jan 20 – Feb 18
 • Mbuzi Capricorn:Des 22 – Jan 19
 • Kondoo Aries: Machi 21 – Aprili 19
 • KaaCancer: Juni 21 – Julai 22
 • Mapacha Gemini: Mei 22 – Juni 20
 • Mashuke Virgo:Agosti 23 – Sept 22
 • Samaki Pisces:Feb 19 – Machi 20
 • Ng’ombe Taurus: Aprili 20 – Mei 21
 • Mizani Libra: Sept 23 – Okt 22
 • Simba Leo: Julai 23 – Agosti 22
 • Ng’e Scorpio: Okt 24- Nov 21