Back

ⓘ Dayolojia ni mazungumzo ya kupokezana kati ya watu wawili au zaidi. Dayolojia huweza kuwa ya ana kwa ana baina ya wazungumzaji au kwa njia ya simu, maandishi n. ..
Dayolojia
                                     

ⓘ Dayolojia

Dayolojia ni mazungumzo ya kupokezana kati ya watu wawili au zaidi.

Dayolojia huweza kuwa ya ana kwa ana baina ya wazungumzaji au kwa njia ya simu, maandishi n.k.

Dayolojia ya ana kwa ana ni mazungumzo ya kupokezana baina ya watu ambao huonana.

Dayolojia inaweza kubuniwa pia. Hapo mtunzi hana budi kujifanya kama mhusika katika dayolojia hiyo.

Katika kutunga dayalojia mtunzi hana budi kujifanya kama mhusika katika dayalojia hiyo. Kwanza anapaswa kutafakari kwa makini mada anayokusudia kuandikia dayalojia, kutayarisha na kupanga mawazo kimantiki na kwa mtiririko na kufikiria wahusika na kuwapangia majukumu kulingana na matendo yao. Kwa mfano kama mhusika ni mkulima, lugha anayopewa, vifaa anavyosemekana kuvitumia na mandhari aliyomo ni lazima vifanane na hali ya mkulima halisi.

Mambo ya kuzingatia katika dayalojia ni pamoja na haya yafuatayo:

  • Pawepo mwingiliano wa mazungumzo ya wahusika na kudakia maneno ili dayalojia iwe na uhalisia.
  • Kuwa na mazungumzo ya mkato na yasiyozidiana sana kati ya wahusika. Mhusika mmoja asitawale mazungumzo kupita wengine.
  • Kutoa maelezo ya ufafanuzi katika mabano ili kumfahamisha
  • Kutumia vihisishi ili kufanya dayalojia iwe ya kusisimua