Back

ⓘ Mstahili heshima ni jina ambalo katika Kanisa Katoliki linatumika hasa kwa muumini aliyefariki ambaye, baada ya kesi kuchunguza uadilifu wake wa kiwango cha ush ..
Mstahili heshima
                                     

ⓘ Mstahili heshima

Mstahili heshima ni jina ambalo katika Kanisa Katoliki linatumika hasa kwa muumini aliyefariki ambaye, baada ya kesi kuchunguza uadilifu wake wa kiwango cha ushujaa, Papa ameuthibitisha rasmi.

Uchunguzi huo unahusu maadili ya Kimungu imani, tumaini na upendo, maadili bawaba pamoja na unyenyekevu. Kwa watawa unachunguzwa pia utekelezaji wa nadhiri zao.

Pamoja na hayo, Kanisa linasubiri Mungu athibitishe mwenyewe kwa muujiza mmoja iliyopatikana kwa maombezi ya huyo ili aweze kutangazwa mwenye heri na wa pili ili atangazwe mtakatifu.