Back

ⓘ Mapigano ya Lepanto yalifanyika baharini tarehe 7 Oktoba 1571 kati ya Wakristo na Waislamu, meli zao zilipokutana katika Ghuba ya Patras. Lepanto ni jina la ban ..
Mapigano ya Lepanto
                                     

ⓘ Mapigano ya Lepanto

Mapigano ya Lepanto yalifanyika baharini tarehe 7 Oktoba 1571 kati ya Wakristo na Waislamu, meli zao zilipokutana katika Ghuba ya Patras. Lepanto ni jina la bandari zilipoondoka meli za Dola la Osmani, wakati zile za mshikamano wa Kikristo zilitokea Messina.

Ni kwamba mwaka 1571 Papa Pius V aliunganisha nchi za Kikatoliki katika "Liga Sancta" ili kuzuia Waturuki wa dola hilo wasiteke Ulaya nzima.

Ingawa jeshi la baharini la Wakristo lilizidiwa na jeshi la Dola la Osmani kwa idadi, walipata ushindi mkubwa. Matokeo yake yakawa ya kudumu: Waturuki hawakuweza kuteka Ulaya magharibi wala kwenda Amerika kupitia bahari ya Atlantiki.

Ushindi huo haukutegemewa, ila uliombwa na Wakatoliki wa Ulaya nzima kwa Rozari, kama alivyoagiza Papa. Pius V aliona ushindi huo umetokana na maombezi ya Bikira Maria akaanzisha sikukuu ya Bibi Yetu wa Ushindi. Mjini Roma mwenyewe aliongoza maandamano ya ibada kwa ajili hiyo.