Back

ⓘ Mashirika - ya ombaomba, Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga, ya kilimwengu, Mtawa, Historia ya Utawa, Ukanoni, Mimutie Women Organization ..
                                               

Mashirika ya ombaomba

Watawa wa kike hawakuweza kufuata mtindo uleule: waliishi kimonaki lakini kwa kuzingatia ufukara na udugu wa Kifransisko na kwa kuombea utume wa hao ndugu wadogo. Klara wa Asizi 1193-1253," mche mdogo” wa Fransisko, ndiye mwanamke wa kwanza kutunga kanuni ya kitawa. Tapo hilo ni maarufu kwa marekebisho yaliyofuatana hadi leo kuhusu ufukara. Tangu karne XII wanawake wengine pia walichangia sana ustawi wa utawa, wa maisha ya Kiroho na wa Kanisa kwa jumla hata kwa maandishi yao. Kati yao Katerina wa Siena 1347-1380, wa utawa wa tatu wa Mt. Dominiko, ametangazwa kuwa mwalimu wa Kanisa.

                                               

Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga

Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga ni umoja wa kimataifa wa kampuni za usafiri kwa ndege. Makao makuu yake yako Montreal, Quebec nchini Kanada ambako kuna pia makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa Kiraia. IATA ilianzishwa mwaka 1945 ili kujenga ushirikiano wa makampuni makubwa ya ndege. Leo hii kuna takriban kampuni wanachama 240. Haya ni hasa makampuni ya kitaifa au makampuni makubwa ya kibiashara yanayotoa huduma za kimataifa. Mashirika madogo yanayohudumia nchi moja tu, pamoja na mashirika ya ndege za kukodi, mara nyingi si wanachama. Kati ya kazi za IATA ni jitihada za kusa ...

                                               

Mashirika ya kilimwengu

Mashirika ya kilimwengu ni mashirika yaliyokubaliwa na viongozi wa Kanisa Katoliki kwa waamini wanaojisikia wito wa kushika mashauri ya Kiinjili kama watawa, lakini si lazima kwa kuishi kijumuia.

                                               

Mtawa

Mtawa ni mtu anayejitenga na ulimwengu ili kuishi maisha maadilifu. Katika dini mbalimbali, mfano mmojawapo wa utawa ni ule wa wamonaki. Lakini katika Ukristo, hasa wa Magharibi historia ya Utawa ilitokeza aina nyingine mbalimbali. Katika Kanisa Katoliki, ni mwamini yeyote aliyejiweka wakfu kwa Mungu hasa kwa kushika useja mtakatifu, lakini kwa kawaida pia ufukara na utiifu. Mara nyingi watawa wanaunda mashirika yenye karama moja inayofafanuliwa na kuratibiwa katika kanuni na katiba maalumu. Mtawa anaweza kuwa mwanamume au mwanamke, mwenye daraja takatifu au la.

                                               

Historia ya Utawa

Hatuwezi kuelewa utawa tukidhani ni kitu kimoja: jina hilo linajumlisha maisha tofautitofauti. Katika makala hii tunataka kufuata historia ya maisha haya katika Ukristo kama kitabu bora kilichoandikwa na Mungu siku kwa siku kadiri ya mpango wake wa hekima kwa ujenzi wa Kanisa lake takatifu kwa karama za kumshuhudia Yesu katika sifa na kazi zake mbalimbali. Kuna hatua kuu nne zilipozaliwa aina mpya za utawa hasa magharibi bila ya kufuta zile zilizotangulia: 3. Kuanzia karne XVI yalitokea mashirika mengi ya kikleri, yasiyo na nadhiri na ya kutolea huduma maalumu. 1. Kuanzia karne III hadi XI ...

                                               

Ukanoni

Ili kuboresha maisha ya mapadri wanajimbo, toka zamani ulisisitizwa uundaji wa jumuia kati yao, ambamo wasali na kufanya utume kwa pamoja. Hasa kuanzia karne XI wengi walifanya hivyo kwenye makanisa makubwa kama mtindo mpya wa kitawa unaosisitiza liturujia ya fahari pamoja na uchungaji. Inavyoweza kueleweka, hao walifuata kanuni ya Agostino wa Hippo na kuitwa Wakanoni. Maarufu zaidi katika yao ni Norbert 1082-1134, mwanzilishi wa Wapremontree. Leo mtindo huo unaendelea katika mashirika mbalimbali, ambayo lakini hayana watu wengi kama aina nyingine za utawa.

                                     

ⓘ Mashirika

  • asasi za kiserikali na asasi zisizo za kiserikali. Hivi ni vyombo au mashirika mbalimbali ya kiserikali yanayojishughulisha na utoaji wa huduma katika
  • ambazo baadhi yake zilifikia kuwa na wamonaki zaidi ya 900. Uanzishaji wa mashirika mapya, kama yale ya Wafransisko na Wadominiko, ulipunguza umuhimu wao
  • shinikizo la biashara au la siasa. Vivyo hivyo, usawa wa mashirika ya habari zinazomilikiwa na mashirika ya conglomerate zaweza kushukiwa katika mwanga wa asili
  • astronomique internationale, UAI ni shirika la kimataifa linalounganisha mashirika ya wataalamu wa astronomia kutoka nchi mbalimbali. Lilianzishwa mwaka
  • wanafuata mapokeo ya Ambrosi wa Milano, au yale ya Lyon, Braga, Toledo na ya mashirika mbalimbali ya kitawa k.mf. Wakartusi na Wadominiko Hivi karibuni waamini
  • 1170 - 1221 hasa wa Shirika la Ndugu Wahubiri alilolianzisha, mojawapo kati ya mashirika ya kitawa ya Kanisa Katoliki, aina ya Ombaomba. Ufupisho wa jina la shirika
  • mengine ya pamoja. Monasteri ni tofauti na konventi, zilizoanzishwa na mashirika ya ombaomba, ambayo wanajumuia wake si wamonaki bali wanaitwa ndugu
  • orodha rasmi lakini isiyodai kuwa kamili, hivi kwamba majimbo, nchi na mashirika vinaweza kuwa na nyongeza maalumu za kwao. Toka zamani jina Martyrologium
  • Hispania liturujia ya Braga huko Ureno na kidogo liturujia ya Lyon huko Ufaransa. Pia baadhi ya mashirika ya kitawa yanatunza liturujia za pekee.
  • na mwenendo wa wahandisi na mashirika ya kandarasi za uhandisi nchini Tanzania, kupitia usajili wa wahandisi na mashirika ya kandarasi ya uhandisi. Bodi
                                               

Mimutie Women Organization

Mimutie Women Organization ni asasi isiyo ya Kiserikali iliyoanzishwa na Rose Njilo kwa ajili ya kuwasaidia na kuwainua wanawake wa jamii ya kifugaji ya Kimaasai katika wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha. Ni shirikia ambalo linafanya kazi ya kuwainua wanawake hasa Wamaasai likiamini kuwa mwanamke akiinuka kiuchumi atakua na kujijengea heshima.

Shirika la Hali ya Hewa ya Dunia
                                               

Shirika la Hali ya Hewa ya Dunia

Shirika la Hali ya Hewa ya Dunia ni asasi ya ushirikiano baina ya serikali mbalimbali duniani ikiwa na idadi ya Nchi wanachama 193. Makao makuu ya shirika ni Geneva, Uswisi. Rais wa mkutano wa Dunia wa hali ya hewa ndiye kiongozi mkuu wa shirika ambaye ni Gerhard Adrian, na mtangulizi wake alikuwa David Grimes. Shirika hili lilianzishwa baada ya lile la Shirika la Kimataifa la Hali ya Hewa, lililoanzishwa mnamo mwaka 1873.

                                               

United African Alliance Community Center

United African Alliance Community Center ni shirika lisilo la kiserikali lililopo mkoani Arusha. Shirika hilo lilianzishwa mwaka 1991 na Pete ONeal pamoja na mke wake Charlotte Hill ONeal kwa malengo ya kuwasaidia watoto pamoja kuendeleza utamaduni. Shirika hilo linapatikana katika wilaya ya Arumeru, nje kidogo ya mji mdogo wa Usa River na wanafunzi ndani ya kituo hiki hujifunza sanaa, kompyuta, ufundi pamoja na lugha ya Kiingereza na elimu hizo hutolewa bila ya malipo

                                               

Vision For Youth

Vision For Youth ni asasi isiyo ya kiserikali yenye makao yake mkoani Arusha, asasi hii hufanya kazi katika maeneo matatu makuu ambayo ni afya,elimu ya uraia,pamoja na kuwainua vijana kiuchumi. V4Y hufanya kazi kwa vijana wenye umri kuanzia miaka kumi tano hadi thelethini na tano.

Users also searched:

...

Tanzania Non Government Organisation National.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri anayeshuhulikia Mashirika. NBC Akaunti ya Hundi kwa Mashirika. Mashirika yasiyo ya Serikali NGOS na asasi za kiraia zilizopata usajili kutoka Wakala wa Usajili wa Leseni na Biashara BRELA na Wakala.


...